Mauzo ya bidhaa kimataifa yalishuhudia mkwamo mwaka 2012: UNCTAD

Kusikiliza /

Mauzo ya bidhaa kimataifa yamekwama

Biashara ya bidhaa zinazouzwa nje ilishuhudia mkwamo mnamo mwaka 2012 baada ya kuongezeka kwa kiasi kikubwa miaka ya 2010 na 2011, kulingana na takwimu za Kamati ya Biashara na Maendeleo katika Umoja wa Mataifa, UNCTAD.Katika nchi zinazoendelea, mauzo ya nje yalipanda kwa asilimia 3.6, ingawa ongezeko hilo lilishuhudiwa katika nchi zinazouza bidhaa za mafutana gesi ya petroli pekee.

Nchi maskini zinazouza bidhaa nyingine zilishuhudia kupungua kwa biashara hiyo kwa asilimia 2.54, huku mauzo ya bidhaa nje ya nchi tajiri yakipungua kwa asilimia 2.75.

Kwa mujibu wa UNCTAD, kabla na baada ya mdororo wa uchumi wa kimataifa mwaka 2008-2009, biashara ya bidhaa zinazouzwa nje ilikuwa kubwa, ingawa mnamo mwaka 2009 biashara hiyo ilishuka kwa asilimia 22.27.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031