Marekani yaipatia WFP ngano kwa ajili ya wakimbizi wa Syria

Kusikiliza /

Marekani yatoa ngano kwa ajili ya watu wa Syria

Meli ya Marekani yenye shehena ya ngano  ya kutosheleza watu zaidi ya Milioni Moja kwa kipindi cha miezi minne imeshusha shehena hiyo kwa ajili ya mgao kwa raia wa Syria ikiwa ni sehemu ya msaada wa dharura wa chakula unaotolewa na Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP.  Ikiwa imebeba tani 25,000 za ngano yenye thamani ya dola Milioni 19 kutoka Marekani, meli hiyo MV Advantage iliwasili kwenye bandari ya Beirut nchini Lebanon April 15 na baadaye sehemu ya ngano hiyo ilikobolewa na kisha kusafirishwa nchiniSyria. 

Meli hiyo imeelekea Uturuki ambako itapakua sehemu ya ngano iliyosalia kwa ajili ya kuisafirisha hadi Syria.

Mratibu mkazi wa WFP kwa ajili ya Syria Muhannad Hadi,alisema kuwa msaada huo umetolewa wakati muafaka hasa wakati ambapo mamia ya familia zikiwa kwenye hali mbaya.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930