Maelfu ya watoto nchini Mali hatarini kupata utapiamlo

Kusikiliza /

Watoto waugua utapiamlo, Mali, UNICEF

Kiasi cha watoto 700,000 nchiniMaliwako hatarini kukubwa na matatizo ya utapiamlo, kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama katika eneo la kaskazini ambako makundi ya waasi yanaendesha harakati za kijeshi.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limesema kuwa hali ya utoaji wa huduma za kijamii kwenye shule pamoja na usambazaji wa maji siyo ya kuridhisha jambo ambalo linaongeza hali ya wasiwasi.

UNICEF imesema kuwa, hata hivyo maeneo mengi ya mijini kumekuwa na uimarikaji wa usambazaji wa huduma za kijamii kunakofanywa na mashirika ya usamaria mwema, lakini kunahitajika kuongeza nguvu ili kurejesha ustawi wa kijamii na kulinda maslahi ya watoto.

Marixie Mercado mmoja wa maafisa wa  UNICEF  amesema kuwa shughuli za usambazaji wa huduma za kibinadamu zinazorota kutokana na kukosa fedha. Shirika hilo limeomba msaada wa dola za Marekani milioni 82 ili kuendesha shughuli zake lakini hadi sasa limefaulu kupata dola milioni 20

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29