Katy Perry aunga mkono juhudi za UNICEF na kutembelea Madagascar

Kusikiliza /

Katy Perry

Mwanamuziki wa kimarekani ambaye ametambulika pia kimataifa katy Perry ametembelea Madagasca ikiwa ni juhudi za kuleta uelewa kuhusiana na hali jumla za watoto katika taifa ambalo bado linaandamwa na hali ya umaskini.

 Madagasca kwa sasa inaanza kuumarika upya kisiasa tangu kujitokeza kwa vute nikivute iliyozuka mwaka 2009 iliyoshuhudiwa baadhi ya wanasiasa wakiondoshwa madarakani kwa nguvu.

Akizungumzia ziara yake hiyo, mwanamuzi huyo ambaye ameunga mkono juhudi za shirika la Umoja wa Mataifa linalosika na watoto UNICEF amesema alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo yale yaliyoko mbali.

Kwa upande mwingine aliishukuru UNICEF kwa kumpa fursa ya kushiriki katika moja ya shughuli zake.

Amesema kuwa katika ziara hiyo alitembelea miradi inayohusu elimu, lishe na masuala ya afya.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031