Jitihada ziongezwe kudhibiti vitisho vya matumizi ya nyuklia: UM

Kusikiliza /

Mjadala kuhusu matumizi ya nyuklia

Huko Geneva, Uswisi siku ya kwanza ya kikao cha maandalizi ya mkutano wa nchi wanachama wa mkataba wa kudhibiti kuenea kwa matumizi ya nyuklia ilitawaliwa na mjadala kuhusu vitisho vya nyuklia vinavyofanywa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea na mpango wa nyuklia wa Iran kama anavyoripoti Jaison Nyakundi.(PKG YA JASON NYAKUNDI)

Jumuiya ya Ulaya imelaani vitishio vya mara kwa mara vya Korea Kaskazini vya matumizi ya nguvu na kulitaka taifa hilo kutupilia mbali mipango yake yote ya zana ya nuklia kuambatana na makubaliano ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Ujumbe wa Marekani unasema kuwa mipango ya nuklia nchini Iran ni tisho kwa kipindi hiki ukisema kuwa taifa la Iran litalaumiwa kutokana na ukiukaji wa makubaliano hayo.

Akiongea wakati wa kuanza kwa mkutano mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoihusika na masuala ya kumaliza silaha Angela Kane ameyashauri mataifa kubuni mazingira yanayoweza kutafuta suluhu la hatari zinazotokana na vitisho vya Korea Kaskazin na Iran.

(CLIP YA ANGELA KANE)

“Hii itasaidia kutatua changamoto kuto kwa visa tofauti kwa sababu itatoa ishara ya kuachana na zana za nuklia na kuharamisha sio tu matumizi ya silaha hizo bali kuwepo kwake. Kati hatua hii kumaliza na kuzuia kusambaa sio njia mbadala. Kile kinachohitajika ni kutekelezwa na nguzo tatu za makubalino za kumaliza zana hizo, kuzuia kusambaa kwake na matumzi ya amani ya zana za nuklia. Makubaliano hayo ya zana za nuklia yalianza kutumika mwaka 1970 kwa lengo la kuzuia kusambaa kwa zana za nuklia an teknolojia yake na kuleta ushirikiano kwenye matumizi ya amani ya nishati ya nuklia. Kile kinachohitajika kwa sasa ni kupiga hatua mbele hata kama itakuwa ya pole pole au ngumu.”

Makubalino hayo ya zana za nuklia yalianza kutumika mwaka 1970 kwa lengo la kuzuia kusambaa kwa zana za kunyuklia an teknolojia yake na kuleta ushirikiano kwenye matumizi ya amani ya nishati ya nuklia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031