Heko wananchi wa Iraq kwa kupiga kura: Ban

Kusikiliza /

Moja ya eneo la kupigia kura

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amepongeza kitendo cha wananchi wa Iraq kupiga kura katika uchaguzi wa viongozi wa majimbo mwishoni mwa wiki.  Bwana Ban amesema kwa kutekeleza haki yao ya kikatiba, wananchi waIraq wamedhihirisha azma yao ya kutakuwa kuwa na nchi ya kidemokrasia.  Amesifu ari waliyokuwa nayo ya kupiga kura licha ya matukio ya awali yaliyokuwa na lengo la kukwamisha uchaguzi huo ikiwemo vitendo vya kigaidi na ghasia zilizosababisha kuuawa kwa baadhi ya wagombea na vitisho kwa wafanyakazi wanaohusika na uchaguzi.  Katibu Mkuu pia ameipongeza tume huru ya uchaguzi nchini Iraqkwa maandalizi yaliojaa weledi kwenye uchaguzi huo na kutoa wito kwa hatua thabiti kuchukuliwa ili uchaguzi ufanyike kwenye majimbo yaliyobakia ya Anbar na Ninewa bila ucheleweshaji wa aina yoyote. Ametoa wito kwa wadau wa kisiasa na uchaguzi nchini Iraq kuendeleza ushirikiano na taasisi zinazohusika na masuala ya uchaguzi nchini humo wakati wa mchakato wote wa uchaguzi ikiwemo usuluhishi wa malalamiko yoyote rasmi kabla matokeo hayajatangazwa. Bwana Ban amesema Umoja wa Mataifa kwa upande wake utaendeleza usaidizi wake kwa tume hiyo huru ya uchaguzi ya Iraq

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930