Hali ya usalama Magharibi mwa Cote d'Ivoire bado si shwari sana: Koenders

Kusikiliza /

Bert Koenders

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Cote D'Ivoire Bert Koenders amesema hali bado si shwari sana Magharibi mwa nchi hiyo licha ya kuwepo kwa utulivu.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Koenders ametaja mambo makuu matatu yanayosababisha hali hiyo kuwa ni migogoro juu ya umiliki wa ardhi, mzozo wa mpaka na Liberia na uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.

Koenders ambaye pia anaongoza Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo, UNOCI amesema wanahitaji kushirikiana na serikali ya Cote d'Ivoire ili iweke sera madhubuti ya vigezo vya kumiliki ardhi.

Kuhusu mzozo wa mpaka amesema kesho kutafanyika mkutano mjini Monrovia, Liberia kujadili mvutano huo.

Kuhusu uchaguzi, Bwana Koenders amesema UNOCI inafanya mambo mawili:

(SAUTI-KOENDERS)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031