Hali ya raia wa Sudan waliojikuta kwenye mapigano yatia wasi wasi.

Kusikiliza /

 

Wakimbizi huko Darfur

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Ali Al-Za'tari amelezea wasiwasi uliopo kutokana na usalama wa raia walionaswa kwenye mapigano kati ya vikosi vya serikali na kundi la Sudan Liberation Army, Mashariki mwa Jimbo la Darfur. Umoja wa Mataifa unasema kuwa watu 36,000  wamepiga kambi karibu na makao ya  ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, UNAMID mashariki mwa Darfur. UNAMID inasema kuwa mashirika ya kibinadamu  hayajafanikiwa kuwafikia wale walioathiriwa na mapigano wala kupata idadi  kamili au haliyao. Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA limetoa ombi la kutaka kufikiwa wathiriwa . Jens laerke ni msemaji wa OCHA.

 (SAUTI YA JENS)

"Kwa sasa hatuwezi kuwafikia hao watu, kwa hiyo tunawasihi wahusika waturuhusu,tuwafikie, kwanza tuweze kufahamu idadi yao na halafu kutambua mahitaji yao ya kibinadamu."

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29