Hali mbaya ya usalama yatatiza huduma muhimu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza /

Hali tete ya usalama yakatiza shughuli CAR

Hali ya usalama kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati inasalia tete ikitatiza jitihada za utoaji wa chakula na mashirika ya kutoa misaada kwenye maeneo yaliayoathiriwa na mizozo nchini humo kwa mujibu wa Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA.Mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa yamepunguza au kufutilia mbali shughuli zao hususan nje ya mji mkuu Bangui. OCHA inasema kuwa watu wote milioni 4.6 kwenye Jamhuri ya Afrika ya kati wameathiriwa na mzozo wakati watu 173,000 wakikimbia makwao.

Marixie Mercado kutoka Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF anasema kuwa  hali iliyopo imetatiza shughuli za masomo na usambazaji wa misaada kutokana na hofu ya kuporwa.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO) 

Huduma za kibinadamu kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa sasa zinakabiliwa na haba wa dola milioni 100.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29