Global Fund kukusanya bilioni 15 kukabili ukimwi, kifua kikuu na malaria

Kusikiliza /

Mfuko wa kimataifa yaani Global fund ambao unapambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria umetangaza kwamba una lengo la kuchangisha dola bilioni 15 ili uweze kuzisaidia ipasavyo nchi katika vita dhidi ya maradhi hayo matatu katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2016.

Global fund imejizatiti kuchagiza mafanikio ya vita dhidi ya ukimwi, kifua kikuu na malaria katika miaka ya hivi karibuni kwa kupitia mikakati  na mipango ya uwekezaji ambayo itaokoa maisha ya mamilioni ya watu na mamilioni ya dola siku za usoni.

Huku ikitambua changamoto zinazozikabili nchi nyingi, mfuko huo na washirika wake wametaja thamani ya fedha zinazowekezwa katika kutoa huduma za afya zinazohitajika.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930