Bi. Robinson akutana na Rais Kabila mjini Kinshasa

Kusikiliza /

Bi. Mary Robinson

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika nchi za Maziwa Makuu barani Afrika Mary Robinson ambaye ameanza ziara yake katika eneo hilo amekuwa na mazungumzo na Rais Joseph Kabila mjini Kinshasa na kupongeza dhima ya serikali katika makubaliano ya kuleta amani, ulinzi na ushirikkiano kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.  Katika mkutano na waandishi wa habari, Bi. Robinson amesema ni matumaini yake kushirikiana na Rais Kabila pamoja na pande zote zilizotia saini makubaliano hayo mjiniAddis Ababa,Ethiopiaili yaweze kutekelezwa kivitendo kwa ajili ya amani ya kudumu mashariki mwa DRC. Mjumbe huyo maalum amesema makubaliano hayo ya nchi 11 yanatoa fursa mpya ya kupatia suluhu mgogoro wa Mashariki mwa DRC kwa kutatua vyanzo vyake kwa maslahi ya wakazi wa nchi hiyo na wale wa Maziwa Makuu. Bi. Robinson amesistiza umuhimu wa ushiriki wa makundi yote katika kuleta amani kweney eneohilona atahitimisha ziara yake DRC siku ya Jumanne kwa kutembelea mji wa Goma ulioko Mashariki mwa nchi hiyo. Ziara hiyo itampeleka piaRwanda,Uganda,Burundi, Afrika Kusini na kuhitimisha huko Ethiopia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2015
T N T K J M P
« ago    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
282930