Baraza la usalama limeongeza muda wa MINURSO Sahara Magharibi:

Kusikiliza /

MINURSO

Katika azimio lililoungwa mkono na wajumbe wote 15 baraza limeelezea hofu yake kuhusu ukiukwaji wa makubaliano ya sasa na kutoa wito kwa pande zote kuheshimu muafaka, wajibu wao na makubaliano ya kijeshi yaliyofikiwa na MINURSO kuhusu usitishaji mapigano.

Baraza pia limezitaka pande zote kushirikiana kikamilifu na MINURSO ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zinazohitajika kuhakikisha usalama wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, kuwapa uhuru wa kutembea na kuzungumza na watu husika na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao bila vikwazo. Baraza limezitaka pande husika pia kuendelea na majadiliano chini ya upatanishi wa Umoja wa Mataifa bila masharti yoyote kwa kuzingatia hatua zilizopigwa tangu 2006 ili kupata suluhu ya kisiasa itakayosaidia eneo hilo la Sahara Magharibi kujitawala.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031