Baraza la usalama lapokea taarifa kuhusu hali halisi Cote d'Ivoire

Kusikiliza /

Edmond Mulet

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepokea ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja huo kuhusu hali halisi ya usalama na amani huko Cote D'Ivoire.Ripoti hiyo iliyowasilishwa na Edmond Mulet, Msaidizi wa Katibu Mkuu katika operesheni za ulinzi wa amani. Ripoti hiyo pamoja na kueleza hali ya usalama kuwa bado si shwari sana, imeibuka na mapendekezo kadhaa ikiwemo kuendelea kuwepo kwa ofisi ya UNOCI ili isaidie nchi hiyo kuimarisha usalama na pia sheria ichukue mkondo wake dhidi ya wakiukwaji wa haki za binadamu.

(SAUTI MULET)

"Kutokana na changamoto hizi na vitisho, uwepo wa UNOCI bado ni muhimu, ukiangalia vipaumbele vyake:kulinda raia, kusaidia marekebisho ya mfumo wa ulinzi, kuchochea upokonyaji silaha na kujumuisha waliokuwa wapiganaji katika jamii na kushughulikia mgogoro wa mpaka."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930