Baraza Kuu lajadili mfumo wa haki dhidi ya jinai na maridhiano

Kusikiliza /

Vuk Jeremic

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala kuhusu nafasi ya mfumo wa kimataifa wa haki kwa makosa ya jinai kwenye maridhiano. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

 (RIPOTI YA ASSUMPTA)

 Ni kwa jinsi gani mfumo wa kimataifa wa haki kwa makosa ya jinai unaweza kuleta maridhiano baada ya mgogoro,hilolilikuwa swali ambapo Rais wa Baraza Kuu la UM Vuk Jeremic aliwaeleza wajumbe kuwa linatakiwa lipatiwe jibu mwishoni mwa mjadala huo. Jeremic amesema maridhiano ni changamoto kubwa kwani yanataka kila upande kuwajibika na yale aliyofanya na kuwa mkweli ili kuepuka madhara yaliyotokea kujirudia na vile vile pande zote kufanya kazi pamoja kwa mustakhabli wa eneo husika na dunia nzima.

 (SAUTI JEREMIC)

 Katibu Mkuu Ban Ki-Moon alihutubia na kusema mfumo wa kutafuta haki kwa makosa ya jinai kupitia mahakama mbali mbali za kimataifa ikiwemo ICC umetoa fursa kwa wahanga kusikika tofauti na zamani. Hata hivyo amesema haki si lazima kutoa adhabu kwa wakosaji, bali kukiri kuwajibika na makosa nako pia kunaweza kusaidia kuepusha uhalifu wa kijinai kutokea tena.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29