Bana matumizi barani Ulaya yatikisa sekta ya umma: ILO

Kusikiliza /

ILO

Hatua zilizochukuliwa na nchi za Ulaya kukabiliana na mdodoro wa uchumi zimeripotiwa kuleta madhara makubwa katika sekta ya umma, na hiyo ni kwa mujibu wa ILO kama anavyoripoti Assumpta Massoi.

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Shirika la kazi duniani ILO limezindua kitabu ambacho kinamulika mshtuko uliokumba sekta ya umma barani Ulaya baada ya hatua za kukabiliana na mdodoro wa uchumi.

Mataifa 30 yalijumuishwa na miongoni mwao 15 yalimulikwa zaidi juu ya hatua walizochukua na madhara yaliyotokea zikiwemo Ugiriki, Romania.

Ureno na Ireland. Hatua hizo ni pamoja na kupunguza ajira, mishahara na marupurupu yaliyokuwa kivutio kwa watu kujiunga na sekta ya umma.

Afisa kutoka ILO, ambaye pia ni mwandishi wa ripoti hiyo Daniel Vaughan-Whitehead amesema athari ni mbaya kuliko ilivyotarajiwa.

 (SAUTI YA DANIEL)

Ili kurekebisha hali hiyo mapendekezo ni kwamba marekebisho ya uchumi yazingatie siyo tu kubana matumizi ya fedha bali pia yazingitie utengamano wa kijamii, mashauriano, fursa za ajira na mazingira ya kazi na ubora wa huduma za umma.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2017
T N T K J M P
« jun    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31