Ban asikitishwa na mauaji ya mlinzi wa amani huko Darfur

Kusikiliza /

UNAMID

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa serikali ya Sudan kuwasaka hadi kuwapata wahusika wa shambulio la leo asubuhi huko Darfur Mashariki lililosababisha kifo cha mlinda amani mmoja kutokaNigeriana kujeruhi wengine wawili. Msemaji wa Ban amemkariri Katibu Mkuu akilaani vikali shambulio hilo lililofanywa na watu wasiojulikana na ametuma rambirambi kwa familia na marafiki wa askari huyo aliyekuwa akihudumu na kikosi cha ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur, UNAMID. Bwana Ban pia ameonyesha wasiwasi wake juu ya vikwazo wanavyokumbana navyo UNAMID katika kupeleka msaada kwa raia walioathirika na mapigano ya hivi karibuni huko Muhajeria na Labado na kutaka mamlaka husika ziviondoe ili misaada iwafikie raia bila vikwazo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2015
T N T K J M P
« ago    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
282930