Ban ashutumu mauaji ya Naibu wakili wa serikali Somalia

Kusikiliza /

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameshutumu mauaji ya Naibu wakili wa serikali nchini Somalia, Ahmed Malim Sheikh Nur yaliyotokea mwishoni mwa wiki mjini Mogadishu na ametua salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu.  Bwana Ban amekaririwa na msemaji wake akieleza wasiwasi wake juu ya mashambulizi ya hivi karibuni yanayoonekana kulenga wafanyakazi wa mahakama na wale wanaohusika na mfumo wa sheria.  Hata hivyo amesema ana imani kuwa vitendo hivyo vya kihalifu havitakwamisha jitihada za kuimarisha utawala wa kisheria nchini humo.

 

Bwana Ban amerejelea tamko lake kuwa Umoja wa Mataifa uko pamoja na serikali ya Somalai na utaendelea kusaidia jitihada za kuimarisha taasisi na wananchi wa Somalia.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2016
T N T K J M P
« apr    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031