Ban apongeza mazungumzo kati ya Bashir na Kiir

Kusikiliza /

Rais Omar Al-Bashir wa Sudan na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameunga mkono mazungumzo yaliyofanyika hii leo huko Juba kati ya marais wa Sudan Omar Al Bashir na Salva Kiir wa Sudan Kusini na kusema anatiwa moyo na majadiliano hayo chanya yenye lengo la kuona makubaliano ya Addis Ababa ya mwezi Septemba mwaka jana yanafikiwa. Bwana Ban amewasihi viongozi hao kuendeleza kasi hiyo huku akiwapongeza kwa uamuzi wao wa kuendeleza jitihada za kupatia suluhu suala la Abyei na kuwasihi wamalize tofauti zao juu ya suluhu ya kudumu ya mzozo huo. Halikadhalika Katibu Mkuu amesifu kuanza tena kwa uzalishaji wa mafuta kama kiashiria kimojawapo cha kurejea kwa uhusiano mwema kati ya Sudan Kusini na Sudan kufuatia kuanzishwa kwa ukanda salama usio wa kijeshi kwenye kwenye mpaka kati yao na kuanza kazi kwa mfumo wa pamoja wa kufuatilia usalama mpakani

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930