Ban alaani vikali mauaji ya walinda amani Sudan Kusini

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameelezea kushtushwa na shambulizi dhidi ya msafara wa walinda amani  wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini mapema Jumanne asubuhi.

Bwana Ban amelaani vikali mauaji ya walinda amani 6 kutoka India na wafanyakazi wengine wawili wa UNMISS raia wa Sudan Kusini, na watano wa kikandarasi, katika eneo la Gumuruk, jimbo la Jonglei, Sudan Kusini.
Wafanyakazi wengine tisa walijeruhiwa katika shambulizi hilo, na baadhi yao wako katika hali mahtuti.

Katibu Mkuu ametoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini iwachukulie walotenda kitendo hicho hatua za kisheria.Amesisitiza kuwa kuwaua walinda amani ni uhalifu wa kivita, chini ya mamlaka ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu.

Bwana Ban ametuma risala ya rambi rambi kwa serikali za India na Sudan Kusini, na familia za walinda amani, wafanyakazi wengine wa UNMISS na wengine wa kikandarasi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2016
T N T K J M P
« jun    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031