Ban akutana na malkia Beatrix wa Uholanzi

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja Umoja wa mataifa Ban Ki-moon leo amekutana na Malkia Beatrix wa Uholanzi. Ban ametoa shukrani zake kwa mchango muhimu unaotolewa na Uholanzi katika kufanikisha kazi za Umoja wa Mataifa.

Pia ameshukuru msaada utolewao na Prince Willem-Alexander na Princess Maxima katika kusaidia miradi ya kimataifa ya maendeleo na juhudi zao za kusaidia ili taifahilona kwengineko kuweza kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

Ban na Malkia pia wamejadili maandalizi ya hafla ya hekalu la amani yaliyopangwa kufanyika Agosti 28 mwaka huu mjini The Hague.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930