Ban afurahia juhudi za kuepusha machafuko Guinea

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha hatua zilizopigwa katika kurejelea mazungumzo ya kisiasa nchini Guinea.Katika taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban amesema ametiwa moyo hasa na kutiwa saini azimio la pamoja baina ya serikali, upinzani na mrengo wa rais mnamo Aprili 23, ambalo linatoa wito kwa pande zote kisiasa kujiepusha na maandamano yoyote yenye ghasia, na kuaihidi kutataua masuala yoyote yenye utata kwa njia ya mazungumzo ya amani.

Katibu Mkuu pia amekaribisha taarifa ilotolewa na Rais Alpha Condé, hii leo Aprili 24, ikitaja kuwa yu tayari kutekeleza kila kitu kitakachohakikisha uwazi na uaminifu wa harakati za uchaguzi, kwa kuhusisha wadau wa kimataifa.

Akiahidi uungwaji mkono kutoka Umoja wa Mataifa, Bwana Ban ametoa wito kwa viongozi wa serikali na upinzani kujadiliana na kukabiliana na changamoto zilizopo katika harakati za uchaguzi ili kulinda amani na utulivu nchini.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031