Nyumbani » 29/04/2013 Entries posted on “Aprili 29th, 2013”

Baraza la usalama lasikitishwa na hali ya usalama Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / Jeffrey Feltman

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeeleza wasiwasi wake mkubwa juu ya kuzidi kuzorota kwa hali ya usalama huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na kutaka mamlaka husika zirejeshe amani, utulivu na usalama kwenye mji mkuu Bangui. Tamko hilo ni kwa mujibu wa taarifa ya Baraza hilo iliyotolewa mwishoni mwa kikao cha mashauriano kuhusu [...]

29/04/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Bi. Robinson akutana na Rais Kabila mjini Kinshasa

Kusikiliza / Bi. Mary Robinson

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika nchi za Maziwa Makuu barani Afrika Mary Robinson ambaye ameanza ziara yake katika eneo hilo amekuwa na mazungumzo na Rais Joseph Kabila mjini Kinshasa na kupongeza dhima ya serikali katika makubaliano ya kuleta amani, ulinzi na ushirikkiano kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, [...]

29/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watanzania waadhimisha miaka 49 ya muungano mjini New York,watoa wito kero za Muungano zitatuliwe

Kusikiliza / Wakati wa mahojiano Balozi Ramadhan Mwinyi na Joseph Msami

  Mwishoni mwa wiki Watanzania wanaoishi mjini New York na vitongoji vyake waliungana na watanzania wengine kuadhimisha miaka 49 ya muungano wa Tanganyika na Zainzibar ulioasisiwa mwaka 1964. Joseph Msami ameandaa makala ifuatayo kufahamu nini kilijiri katika siku hiyo.

29/04/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Wanajeshi Mali wapewa mafunzo

Kusikiliza / wANAJESHI WAPEWA MAFUNZO, Mali

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la wakimbizi, UNHCR , pamoja na ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA yameendesha mafunzo kwa askari na wanajeshi nchini Mali kuhusu haki za binadamu na sheria za kimataifa. Mafunzo hayo yameandaliwa kuwawezesha maafisa wa jeshi kuelewa tofauti kati ya wapiganaji na raia, ulinzi dhidi ya wafanyakazi wa [...]

29/04/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Hifadhi ya jamii ni muhimu katika kuondoa ajira kwa watoto

Kusikiliza / ILO_logo

Shirika la kazi duniani, ILO limetoa ripoti inayoeleza bayana kuwa sera bora za hifadhi ya jamii ni nguzo ya kuondokana na ajira kwa watoto. Ufafiti huo ulioangazia udhaifu wa kiuchumi, hifadhi ya kijamii na vita dhidi ya ajira kwa watoto ulihusisha nchi mbali mbali ikiwemo Tanzania, Botswana, Malawi na Namibia ambapo kipato miongoni mwa wazee [...]

29/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ameteua Kay kumwakilisha huko Somalia, anachukua nafasi ya Balozi Mahiga

Kusikiliza / Augustine Mahiga

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemteaua Nicholas Kay wa Uingereza kuwa mwakilishi wake maalum huko Somalia, akichukua nafasi ya Balozi Augustine Mahiga kutoka Tanzania anayemaliza muda wake mwezi Juni mwaka huu. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nersiky amemkariri Bwana Ban akimpongeza Balozi Mahiga kwa uongozi wake wa mfano na wa kujituma [...]

29/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNMISS yakaribisha azimio la amani Sudan Kusini

Kusikiliza / Walinda amani wa UNMISS

  Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, umekaribisha azimio la amani baina ya seikali ya Sudan Kusini na makundi yenye silaha nchini humo. Katika taarifa ilotolewa siku ya Ijumaa, kundi la South Sudan Liberation Army (SSLA), na lile la South Sudan Democratic Army (SSDA) na South Sudan Defense Forces (SSDF) yalitangaza kuwa [...]

29/04/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

ILO kupeleka ujumbe Bangladesh kufuatia kuporomoka kwa jingo la Rana Plaza

Kusikiliza / Jengo lililoporomoka

Shirika la kazi duniani ILO linatapeleka ujumbe wa ngazi za juu nchini Bangladesh katika siku chache zijazo ili kusaidia na kuharakisha hatua za kila upande zinazohitajika kufuatia kuporomoka kwa jingo laRana Plaza mjini Savar lililokatili maisha ya watu 380 na wengine wengi kujeruhiwa.Ujumbe huo utaongozwa na naibu mkurugenzi mkuu wa ILO anayehusika na operesheni za [...]

29/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM wakaribisha mazungumzo ya kumaliza uhasama, Iraq, Kurdistan

Kusikiliza / UNAMI

Iraq na Kurdistan zimeanzisha majadiliano kwa shabaha ya kumaliza mivutano ya muda mrefu huku Umoja wa Mataifa ukiamini kupatikana kwa suluhu ya kudumu. Maafisa wa pande zote mbili wamekutana kabla ya mawaziri wakuu kuwa na mkutano wao siku ya jumanne, mjini Bagdad. Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Martin Kobler UNAMI amesema kuwa, [...]

29/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Modibo Toure kuwa Mshauri Maalum wa mjumbe wake wa Maziwa Makuu

Kusikiliza / Bw. Modibo Toure

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amemteua Bwana Modibo Toure kama Mshauri Maalum wa Mjumbe wake katika ukanda wa Maziwa Makuu, Mary Robinson.Tangu mwezi Januari mwaka huu, Bwana Toure ambaye ni raia wa Mali, amekuwa akihudumu kama mratibu mkaazi wa masuala ya kibinadamu na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa mjini Nairobi, Kenya. [...]

29/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Harakati za kudhibiti mabadiliko ya tabianchi zashika kasi

Kusikiliza / Christiana Figueres

Huko Bonn, Ujerumani mazungumzo yameanza hii leo chini ya sekretariati ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, (UNFCCC), kuangalia hatua za kuchukua kudhibiti ongezeko la utoaji wa hewa chafuzi zinazoongeza kiwango cha joto duniani.Mkutano huo unalenga kujadili fursa mbali mbali kuelekea makubaliano kuhusu hali ya hewa yatakayofikiwa kwenye mkutano [...]

29/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Syria iruhusu uchunguzi katika madai ya kutumika silaha za kemikali: Ban

Kusikiliza / Ban Ki-moon na Åke Sellström

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameitaka serikali ya Syria iruhusu uchunguzi wa madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchini humo bila kuchelewa na bila masharti. Joshua mmali na maelezo zaidi (PKG JOSHUA MMALI) Akiandamana na mtaalam msimamizi wa timu ya uchunguzi huo, Dr. Åke Sellström, Bwana Ban amewaambia waandishi wa [...]

29/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Brazil yatoa msaada mkubwa wa chakula kwa wapalestina

Kusikiliza / Brazil yatoa msaada kwa Palestina

Jimbo la Brazil ambalo ni mzalishaji mkubwa wa mpungua la Rio Grande do Sul, kupitia serikali kuu limetoa msaada wa tani 11.500 za mchele kwa shirika la Umoja wa mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA).   Tangazo la msaada huo limetolewa na gavana wa Rio Grande do Sul, bwana Tarso Gerno mjini Jerusalem [...]

29/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNESCO na washirika kusaidia kuboresha elimu kwa wote

Kusikiliza / UNESCO yatia saini kwa lengo la kufanikisha elimu ya msingi

Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO ambalo limetiliana saini na shirika linalohusika na elimu ya msingi Educate A Child for Quality Primary Education kwa lengo la kufanikisha lengo la milenia la elimu kwa wote. Makubaliano yametiwa saini leo hukoDoha kama anavyoripoti George Njogopa.(TAARIFA YA GEORGE) Ushirikiano huo unalenga kutoa msukumo [...]

29/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Suluhu la kisiasa Darfur bado kupatikana: Ladsous

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo limeleezwa kuwa miaka Kumi tangu mzozo wa Darfur utambulike kimataifa bado suluhu ya kisiasa haijapatikana na hali ya usalama kwa watendaji wa Umoja wa Mataifa inatia wasiwasi. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.(TAARIFA YA ASSUMPTA) Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataifa [...]

29/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wazindua kampeni ya changamoto ya kutokomeza njaa Asia-Pacific

Kusikiliza / Kampeni kwa lengo la kutokomeza njaa, Asia-Pacific

Umoja wa mataifa Jumatatu umezindua kampeni ya changamoto ya kutokomeza njaa kwenye ukanda wa Asia na Pacific. Alice Kariuki na taarifa zaidi(RIPOTI YA ALICE KARIUKI) Kamepeni hiyo iliyozinduliwa mjini Bangkok Thailand na kuhudhuriwa na viongozi wa kitaifa wa ukanda huo inazitaka serikali, wakulima, wanasayansi, wafanya biashara,jumuiya za kijamii na walaji kushirikiana kutokomeza tatizo la njaa [...]

29/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yaongoza mikakati ya kupambana na ugonjwa wa surua nchini Cambodia

Kusikiliza / Mipango ya kupambana na surua yaimarishwa, Cambodia

Taifa la Cambodia limeongeza maradufu idadi ya watoto wanaopata chanjo dhidi ya ugonjwa wa surua kwa muda wa miaka kumi iliyopita. Hadi mwaka 2011 asilimia 20 ya watoto wote nchini Cambodia hawakuwa wanapata chanjo wanayohitajika ili kujikinga dhidi ya ugonjwa wa surua. Mwaka 2011 shirika la afya duniani WHO lilitoa mchango kwa programu ya kitaifa [...]

29/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tuwaenzi wahanga kwa kutokomeza silaha za kemikali: Ban

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

  Kutokomeza silaha za kemikali na silaha zingine zote za mauaji wa halaiki ndiyo njia bora ya kuwaenzi wahanga wa silaha hizo na kuvikomboa vizazi vijavyo kutokana na hatari ya silaha hizo. Ujumbe huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo Aprili 29, ambayo ni siku ya kimataifa ya kuwakumbuka waathiriwa [...]

29/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma za posta kurejea Somalia, baada ya kukosekana kwa miaka 23

Kusikiliza / Somalia yarejea huduma za posta

Somalia imetiliana saini na falme za kiarabu makubaliano ya kusaidia urejeshaji wa huduma za posta nchini humo baada ya kukosekana kwa miaka 23 kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe.Makubaliano yalitiwa saini kwenye makao makuu ya UPU nchini Uswisi na ambapo kwa mujibu wa makubaliano hayo, mji wa Dubai utakuwa kitovu cha kupokea barua zote [...]

29/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930