Nyumbani » 26/04/2013 Entries posted on “Aprili 26th, 2013”

Hali ya Iraq inatisha, hatua za haraka zichukuliwe – Kobler

Kusikiliza / Martin Kobler

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Martin Kobler, ametaka pande zote nchini Iraq kujizuia na mapigano na badala yake kuwepo kwa mjadala mkuu nchini humo kufuatia mapigano ya hivi karibuni yaliyosababisha vifo na majeruhi kwa mamia ya watu nchini humo. Bwana Kobler ameelezea hofu yake juu ya nchi kuelekea kusikojulikana [...]

26/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM watenga fedha za kukabiliana na hali mbaya ya kibindamu Chad

Kusikiliza / CHAD2

Shirika la UM la kuratibu misaada ya kibinadamu (OCHA) limesema kuwa UM umetenga dola milioni tano za kukabiliana na hali mbaya ya kibinamadu nchini Chad. Fedha hizo zitatumika kukidhi mahitaji ya dharura ya wakimbizi wa Sudan na wahamiaji kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati. Jens Laerke ni msemaji wa OCHA. (SAUTI YA JENS LAERKE) Fedha [...]

26/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Licha ya changamoto, Burundi yapiga hatua kumstawisha mwanamke

Kusikiliza / Wanawake nchini Burundi

Ikiwa zimesalia chini ya siku Elfu Moja kabla ya ukomo wa Malengo ya Milenia mwezi Disemba mwaka 2015, Burundi  yaelezwa kuwa imepiga hatua kubwa katika  moja wapo ya malengo hayo hususan lile la usawa wa kijinsia kwa kuweka mazingira ya usawa kati ya wanawake na wanaume katika Nyanja mbali mbali. Katiba ya nchi hiyo imewatengea [...]

26/04/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM kutoa mafunzo kwa wahamiaji wa Afrika walioko ughaibuni

Kusikiliza / Jumbe Omari Jumbe

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, liko katika mpango maalum unaolenga kutoa mafunzo kwa wahamiaji wa Afrika wanaoishi ughaibuni ili wasaidie maendeleo katika nchi zao kulingana na ujuzi walionao. Katika mahojiano na mwandishi wetu Joseph Msami msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe anasema mpango huo utahimizwa katika nchi mbalimbali baada ya kuonekana una mafanikio na [...]

26/04/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

IOM kuwezesha wasomali walioko Uingereza kuchangia maendeleo ya nchi yao

Kusikiliza / Shirika la IOM kusaidia wasomali kuchangia katika maendeleo

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM kuwawezesha wahamiaji wa kisomali nchini Uingereza kushiriki maendeleo ya nchi yao kama anavyo ripoti Alice Kariuki.  (RIPOTI YA ALICE) Wahamiaji hao wa kisomali walioko Uingereza watapatiwa mafunzo na IOM kwa lengo la kusaidia ustawi wa uchumi wa nchi yao ambayo kwa miongo kadhaa imekuwa katika migogoro.  Hatua hiyo  ya [...]

26/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi kutoka Syria ni mzigo mkubwa kwa UNHCR na majirani zake

Kusikiliza / Mzigo wa kutoa huduma za afya ni mzito

 Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR laeleza  kuzidiwa uwezo wa kutoa huduma za tiba kwa wakimbizi wa  Syria kama anavyoeleza  Jason nyakundi.  (PKG YA JASON NYAKUNDI)Kukiwa na zaidi ya wakimbizi milioni moja nchini Iraq, Jordan na Lebanon shughuli za utoaji huduma za kiaya kwenye nchi hizi zimekumbwa na changamoto kutokana  na kuongezeka idadi ya wakimbizi [...]

26/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali mbaya ya usalama yasababisha ukosefu wa chakula Mali:WFP

Kusikiliza / Ukosefu wa chakula ni tishio kasakazini, Mali

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP linasema hali ya ukosefu wa chakula inazidi kuwa tishio kaskazini mwa nchi hiyo kutokana na kuzorota kwa usalama.WFP inasema hali ni mbaya zaidi katika jimbo la Mopti ambako hata ustawi wa kijamii umezorotakamaanavyoripoti George Njogopa. (PCKG YA GEORGE) Ukosefu wa chakula ni tatizo linalosalia katika eneo la Kaskazini [...]

26/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu la UM lapitisha azimio kuhusu amani barani Afrika

Kusikiliza / Barza Kuu limepitisha azimio kuhusu amani,Afrika

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limerithia azimio la kisiasa kuhusu utatuaji wa mizozo barani Afrika kwa njia ya amani. Assumpta Massoi na taarifa kamili:(TAARIFA ASSUMPTA) Azimio hilo linalohusiana na mkutano wa siku mbili wa Baraza Kuu kuhusu utatuaji wa mizozo kwa njia ya amani barani Afrika, linataja umuhimu wa kuongeza ushirikiano kati ya [...]

26/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Miaka 27 baada ya zahma ya Chernobly athari bado zipo:Ban

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anasema wakati leo dunia ikikumbuka zahma ya Chernobly miaka 27 iliyopita ni muhimu kuwaenzi wafanyakazi wa huduma za dharura waliosaidia wakati wa ajali hiyo ya nyuklia mbaya kabisa kuwahi kutokea na kukatli maisha ya watu wengi huku zaidi ya 330,000 kulazimika kuzihama nyumba zao. Anasema mamilioni [...]

26/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban azungumza na Rais wa Equatorial Guinea

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na Rais wa Equitorial Guinea Obiang Nguema Mbasogo

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mazungumzo na Rais Obiang Nguema Mbasogo wa Equatorial  Guinea ambapo amemshukuru Rais nguema mwa mchango wake katika utatuzi wa mizozo kwa njia ya amani barani afrika. Viongozi hao  wawili walijadiliana kuhusu ushirikiano uliopo kati ya Umoja wa Mataifa na taifa la Equatorial Guinea na jitihada [...]

26/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban azungumzia taarifa za Marekani kuhusu silaha za kemikali Syria

Kusikiliza / Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Msemaji wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon ana taarifa juu ya barua ambayo Ikulu ya Marekani imewasilisha katika baraza la Kongresi kuhusu matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria.  Bwana Ban anachukulia kwa umakini taarifa hizo lakini Umoja wa Mataifa hauwezi kutoa maoni yoyote kwa kuzingatia upelelezi uliofanywa na taifa fulani. Badala [...]

26/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya wakimbizi 30,000 wamewasili nchini Yemeni ndani ya mwaka huu

Kusikiliza / Idadi ya wakimbizi ambao wamewasili Yemen ni kubwa

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limesema kuwa kiasi cha wakimbizi na wahamiaji 30,000 wamewasili nchini Yemen hadi kufikia sasa. Wengi wa wahamiaji hao wanaripotiwa ni wenye uraia wa Ethiopia na kiasi kidogo ni kutoka Somalia. Pia kuna wengine kutoka nchi kadhaa za kiafrika. UHHCR inasema kuwa, katika kipindi cha kuanzia mwaka [...]

26/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP yakabiliana na utapiamlo Madagascar:

Kusikiliza / madagascarfood

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linashughulikia matatizo ya utapia mlo na usalama wa chakula ambayo ni changamoto kubwa kwa taifa hilo. WFP inatumia program maalumu za kitaifa na operesheni za misaada.Lengo kubwa ni kupunguza tatizo sugu la usalama wa chakula kusaidia elimu ya msingi na lishe na kuboresha mikakati ya kukabiliana na [...]

26/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031