Nyumbani » 25/04/2013 Entries posted on “Aprili 25th, 2013”

Ugonjwa wa Malaria bado ni tatizo nchini Burundi

Kusikiliza / mosquitoes

Wakati siku ya Malaria duniani ikiangaziwa tarehe 25 Aprili na ujumbe Wekeza kwa baadaye tokomeza Malia, nchini Burundi takwimu zinayonesha kuwa asilimia 21 ya wananchi husumbuliwa na maradhi hayo. Ugonjwa huo umekuwa tatizo la kwanza la afya. Wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano ndio wanaathiriwa sana na Malaria. Lakini takwimu za mwaka [...]

25/04/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wakaribia kupeleka ujumbe wa UNAMSOM Somalia

Kusikiliza / somalia-map1

Umoja wa Mataifa unaendelea kufanya kazi na serikali ya Somalia na mamlaka za mikoa ili kuweka ujumbe mpya wa Umoja wa Mataifa wa kuisaidia Somalia, UNAMSOM, kwa ajili ya kuendeleza amani na kulijena tena taifa hilo, kama lilivyoazimia Baraza la Usalama katika azimio namba 2093 (2013). Akilihutubia Baraza la Usalama hii leo, Mkuu wa Masuala [...]

25/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama limeongeza muda wa MINURSO Sahara Magharibi:

Kusikiliza / MINURSO

Katika azimio lililoungwa mkono na wajumbe wote 15 baraza limeelezea hofu yake kuhusu ukiukwaji wa makubaliano ya sasa na kutoa wito kwa pande zote kuheshimu muafaka, wajibu wao na makubaliano ya kijeshi yaliyofikiwa na MINURSO kuhusu usitishaji mapigano. Baraza pia limezitaka pande zote kushirikiana kikamilifu na MINURSO ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zinazohitajika kuhakikisha [...]

25/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ali Al-Za'tari akaribisha mazungumzo ya amani ya Sudan

Kusikiliza / Al-Zahtari

Mwakilishi Mkaazi wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Ali Al-Za’tari ameungana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon katika kukaribisha mazungumzo ya moja kwa moja kati ya serikali ya Sudan na kundi la Sudan People’s Liberation Movement North yanayofanywa chini ya mwavuli wa Jopo [...]

25/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laamuru ujumbe wa kuweka udhibiti Mali, MINUSMA

Kusikiliza / Ujumbe wa MINUSMA,Mali

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limepitisha mswada unaoamuru kupelekwa vikosi vya kulinda amani nchini Mali, na kubadilishwa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo kuwa ujumbe wenye umbo mseto wa kuimarisha udhibiti, MINUSMA, ambao utahitajika kuanza kajukumu yake mnamo tarehe 1 Julai mwaka 2013. Joshua Mmali na taarifa kamili  (TAARIFA YA [...]

25/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kundi la Séléka lazidi kudidimiza haki za watoto: Zerrougui

Kusikiliza / Leila zerrougui

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa watoto walionaswa katika maeneo ya mizozo Leila Zerrougui ameonyesha wasiwasi wake juu ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za watogo vinavyofanywa na vikundi vyenye silaha vya kundi la Séléka huko Jamhuri ya Afrika ya Kati. Katika taarifa yake amesema kumekuwepo na ripoti kuwa takribani katika [...]

25/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Afrika isaidiwe kutatua mizozo kwa njia ya amani: Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Juhudi za kutatua mizozo kwa njia ya amani, Afrika

Juhudi za kutatua mizozo kwa njia ya amani,Afrika Ulimwengu unatakiwa kujitolea, na kwa ari zaidi, ili kusaidia kumaliza migogoro ambayo imeendelea kuyakatili maisha ya watu wengi barani Afrika. Kauli hiyo imetolewa na rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Vuk Jeremic, wakati wa kikao maalum cha Baraza hilo kinachoangazia suala la utatuzi wa mizozo [...]

25/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa haki za binadamu wa UM kukusanya taarifa za wakimbizi wa Eritrea

Kusikiliza / Kambi ya wakimbizi

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Eritrea Sheila B. Keetharuth, atafanya ziara ya kikazi Ethiopia na Djibouti kuanzia tarehe 30 Aprili hadi 9 May 2013 ili kukusanya moja kwa moja taarifa kutoka kwa wakimbizi wa Eritrea kuhusu hali ya haki za binadamu nchini mwao. Amesema kutokana na kutokuwa [...]

25/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mustakhbali wa nyuklia wajadiliwa na mawaziri Petersburg:IAEA

Kusikiliza / Mawaziri kukutana kujadili mustakhbali wa nyuklia

Mawaziri wa serikali mbalimbali na wataalamu wa kimataifa wanakutana mjini Persburg Urusi kuanzia June 27 hadi 29 mwaka huu kujadili mustakhbali wa nyuklia. Maelezo zaidi na George Njogopa (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA) Kongamano hilo linashabaha ya kutoa fursa kwa watunga sera pamoja na wataalamu wengine kujadilia kwa kina nafasi na uwezekano wa matumizi ya nguvu za [...]

25/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukanda wa Zambezi wazindua juhudi za kuondoa Malaria

Kusikiliza / Mpamgo wa kuondoa malaria wazinduliwa, ukanda wa Zambezi

Katika kuadhimisha siku ya Malaria duniani hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe na kusema kuwa bado ugonjwa huo ni mzigo kwa nchi maskini hususan barani Afrika ambako mamilioni ya watu wanashindwa kujikinga dhidi ya Malaria. Amesema barani Afrika kila dakika mtoto mmoja hufariki dunia kutokana na Malaria na kwamba mifumo [...]

25/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO , UNICEF wazindua mpango wa kuangamiza ugonjwa wa polio

Kusikiliza / Mpango wa miaka sita awa kuangamiza Polio

Shirika la Afya Duniani WHO kwa ushirikino na Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF wameibuka na mkakati wa  miaka sita wenye lengo la kuangamiza ugonjwa wa polio Mpango huu unalenga kutoa chanjo hasa nchini Afghanistan, Pakistan na Nigeria ambapo visa vya ugonjwa huu viko juu. Jason Nyakundi ameandaa taarifa hii (PKG YA JASON NYAKUNDI) [...]

25/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vyandarua ni muhimu katika kupunguza vifo vitokanavyo na Malaria: UNICEF

Kusikiliza / Mama akiwa amelala kwenye chandarua

Ugonjwa wa Malaria unaua watu Laki Sita na sitini kila mwaka na wengi wao ni watoto barani Afrika, lakini iwapo kila mtu duniani ataweza kutumia vyandarua vyenye viuatilifu tunaweza kuishinda Malaria. Huo ni ujumbe wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF hii leo katika kuadhimisha siku ya Malaria duniani.  UNICEF na washirika [...]

25/04/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Siku ya Malaria duniani, bado Afrika yazidiwa mzigo: Ban

Kusikiliza / Siku ya Malaria duniani

Katika kuadhimisha siku ya Malaria duniani hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe na kusema kuwa bado ugonjwa huo ni mzigo kwa nchi maskini hususan barani Afrika ambako mamilioni ya watu wanashindwa kujikinga dhidi ya Malaria.  Bwana Ban amesema barani Afrika kila dakika mtoto mmoja anafariki dunia kutokana na ugonjwa [...]

25/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031