Nyumbani » 24/04/2013 Entries posted on “Aprili 24th, 2013”

Watoto Somalia waanza kupatiwa chanjo dhidi ya magonjwa hatari

Kusikiliza / Mtoto akipatiwa chanjo

Serikali ya Somalia imezindua utoaji wa chanjo yenye mchanganyiko wa kinga dhidi ya magonjwa matano hatari kwa watoto walio na umri wa chini ya mwaka mmoja na hivyo kuokoa maisha ya maelfu ya watoto.  Chanjo hiyo ni kinga kwa magonjwa kama vile dondakoo, pepopunda, kifaduro, homa ya ini aina ya B na numonia na itakuwa [...]

24/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Amani maziwa makuu barani Afrika kumulikwa wakati wa ziara ya Mary Robinson

Kusikiliza / Bi. Mary Robinson

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za Maziwa Makuu barani Afrika, Mary Robinson atakuwa na ziara ya wiki moja kwenye ukanda huo kuanzia tarehe 29 mwezi huu.  Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Martin Nersiky amewaambia waaandishi wa habari mjiniNew York, kuwa ziara hiyo ya kwanza kufanywa na Bi. Robinson akiwa [...]

24/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ukatili wa kijinsia bado tatizo Angola- Pillay

Kusikiliza / Angola inapaswa kutokomeza ukatili haswa wa kijinsia, Pillay

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Navi Pillay, amesema licha ya hatua za maendeleo zilizopigwa na Angola ikiwa ni miaka kumi baada ya kukomesha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, nchi hiyo inapaswa kutokomeza ukatili hususani wa kijinsia unaofanywa na vikosi vya ulinzi na maafisa wa uhamiaji. Akitoa majuimuisho ya zaiara yake [...]

24/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tunaweza kushinda vita dhidi ya Malaria Global Fund

Kusikiliza / Global Fund

Mfuko wa kimataifa wa kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria yaani Global Fund umesema leo kwamba hatua mpya katika upande wa kisayansi na utekelezaji wake vimetoa fursa kwa jamii ya kimataifa kudhibiti malaria na kuiondoa katika orodha ya maradhi tishio katika afya ya dunia. Wakati mataifa mengi yakiadhimisha siku ya afya duniani hapo kesho [...]

24/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban afurahia juhudi za kuepusha machafuko Guinea

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha hatua zilizopigwa katika kurejelea mazungumzo ya kisiasa nchini Guinea.Katika taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban amesema ametiwa moyo hasa na kutiwa saini azimio la pamoja baina ya serikali, upinzani na mrengo wa rais mnamo Aprili 23, ambalo linatoa wito kwa pande zote kisiasa kujiepusha na [...]

24/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Asia-Pasific kinara wa matumizi ya malighafi -UNEP

Kusikiliza / Shirika la UNEP kuhusu Asia, Pacific

Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP, inaonyesha ukanda wa Asia- Pasific unaongoza duniani kwa matumizi ya malighafi na kwamba utaendelea kuwa kinara katika matumizi hayo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa leo, uwiano wa biashara katika ukanda wa Asia-Pacific unaonyesha kwamba kiwango cha sasa cha matumizi ya rasilimali hakitoshi kusaidia [...]

24/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tathmini ya ugonjwa wa homa ya mafua ya ndege China yakamilika

Kusikiliza / Uchunguzi wa homa ya mafua ya ndege

Jopo la wataalamu wa kimataifa na wa China lililofanya ziara ya kutathmini hali ya ugonjwa wa mafua ya ndege aina ya H7N9 nchini humo na hatimaye kutoa mapendekezo limehitimisha kazi yake ambapo kwa kiasi kikubwa limesema hatua zilizochukuliwa kudhibiti ugonjwa huo zinatia moyo.  Ziara hiyo ilifanyika katika majimbo ya Shanghai naBeijingambapo Mkurugenzi msaidizi kutoka Shirika [...]

24/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Chanjo ni njia bora na rahisi kulinda maisha ya watoto:Ban

Kusikiliza / Wiki ya chanjo

  Wiki ya chanjo duniani  ni fursa muhimu ya kuchagiza jamii kuhusu haja ya kuwalinda watoto kutokana na chanjo dhidi ya magonjwa yanayozuilikakamapolio, surua na pepo punda. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe maalumu wa wiki ya chanjo duniani kwenye hafla iliyoandaliwa na  Pan American Health Organization hukoBelize. [...]

24/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Suala la Mashariki ya Kati lamulikwa tena na Baraza la Usalama

Kusikiliza / Baraza la Usalama kuhusu Syria

Mizozo na harakati za amani Mashariki ya Kati vimemulikwa tena na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wiki moja baada ya Baraza hilo kuelezwa kwa kina kuhusu baa linaloibuka nchini Syria, wakati mgogoro unapoendelea kutokota. Grace Kaneiya na taarifa kamili(TAARIFA YA KANEIYA) Kikao cha leo cha Baraza la Usalama pia kimehudhuriwa na kuhutubiwa na [...]

24/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Afrika lazima iboreshe bidhaa za viwandani ili kukuza uchumi na kumaliza umasikini

Kusikiliza / Kuboresha bidhaa viwandani kutainua uchumi, Afrika

Ripoti kuhusu hali ya uchumi barani Afrika inasema nchi za bara hilo zina fursa ya kuboresha na kubadili uchumi wake kwa kupitia bidhaa za viwandani kutokana na rasilimali nyingi zilizopo barani humo.Ripoti inasema Afrika itaweza kukabiliana na bei kubwa ya bidhaa kwa sasa na kubadili mfumo wa uzalishaji kimataifa, kama inavyofafanua zaidi ripoti hii ya [...]

24/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bahrain yafuta ziara ya mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu utesaji

Kusikiliza / Bahrain yafungia mlango mtaalamu wa UM

Matarajio ya mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya utesaji Juan E. Méndez kufanya ziara ya uchunguzi hukoBahrain  kuanzia tarehe Nane mwezi ujao yamepeperuka baada ya serikali ya nchi hiyo kuamua kuahirisha ziara yake kamaanavyoripoti George Njogopa. Hii ni mara ya pili kukatishwa kwa ziara ya mtaalamu huyo na yeye mwenyewe amesema kuwa pamoja [...]

24/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WHO yachukua hatua kudhibiti usugu wa dawa dhidi ya Malaria

Kusikiliza / Hatua zimepigwa katika kupigana na Malaria

Wakati dunia kesho inaadhimisha siku ya Malaria duniani, Shirika la afya duniani, WHO pamoja na kutambua mafanikio ya kukinga na kudhibiti malaria kwenye nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, limeamua kuangazia usugu wa dawa za Malaria huko ukanda wa Kusini Mashariki mwa Asia eneo la Mekong kama anavyofafanua Dr Thomas Teuscher chanjo [...]

24/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tume ya UM ya kulipa fidia yailipa Kuwait dola bilioni 1.13

Kusikiliza / Kuwait imelipwa dola bilioni 1.13 na tume, UM

Tume ya Umoja wa mataifa ya fidia leo imetoa dola bilioni 1.13 kwa ajili ya kuilipa Kuwait ikiwa ni sehemu ya madai yaliyosalia ya nchi hiyo.Kwa malipo hayo tume sasa itakuwa imeshalipa dola bilioni 41.2 ya jumla ya dola bilioni 52.4 ilizoahidi kwa mataifa zaidi ya 100 na mashirika ya kimataifa kufuatia madai zaidi ya [...]

24/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Bana matumizi barani Ulaya yatikisa sekta ya umma: ILO

Kusikiliza / ILO

Hatua zilizochukuliwa na nchi za Ulaya kukabiliana na mdodoro wa uchumi zimeripotiwa kuleta madhara makubwa katika sekta ya umma, na hiyo ni kwa mujibu wa ILO kama anavyoripoti Assumpta Massoi. (TAARIFA YA ASSUMPTA) Shirika la kazi duniani ILO limezindua kitabu ambacho kinamulika mshtuko uliokumba sekta ya umma barani Ulaya baada ya hatua za kukabiliana na [...]

24/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mratibu wa UM wa masuala ya kibinadamu Somalia azuru Bosasso

Kusikiliza / Mratibu mpya, UM azuru Bosaso, Somalia

Mratibu mpya mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Philippe Lazzarini ambaye anazuru Somalia kwa mara ya kwanza tangu kushika wadhifa huo mapema mwezi huu amezuru mji wa Bosasso Kaskazini Mashariki mwa Puntland siku ya Jumanne.Baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Bwana Lazzarini alilakiwa na maafisa wa serikali, maafisa kutoka wizara ya afya na [...]

24/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031