Nyumbani » 23/04/2013 Entries posted on “Aprili 23rd, 2013”

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi kwa ubalozi wa Ufaransa nchini Libya

Kusikiliza / Baraza la Usalama

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani vikali shambulizi dhidi ya ubalozi wa Ufaransa mjini Tripoli leo April 23, na kutuma risala ya pole kwa familia na wahanga. Katika taarifa ilotolewa na msemaji wake, Bwana Ban amesema mshambulizi dhidi ya balozi za kigeni na wafanyakazi wake hayakubaliki. Taarifa hiyo pia inasema Katibu [...]

23/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Leo ni siku ya kimataifa ya vitabu na hati miliki:UNESCO

Kusikiliza / Ni siku ya umhuhimu na uwezo wa vitabu

Leo ni siku ya Kimataifa ya vitabu na hati miliki . Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO limekuwa likiadhimisha siku hii kila tarehe 23 April kwa miaka 17 sasa.Nchi wanachama wa UNESCO wanaadhimisha siku hii kwa kutambua umuhimu na uwezo wa vitabu kuwaleta watu pamoja na kuelimisha kuhusu utamaduni [...]

23/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM kuisaidia Uchina kuondosha chembechebe zinazoathiri tabaka la ozoni

Kusikiliza / Tabaka la ozoni

Bodi ya Umoja wa Mataifa ambayo imeundwa kwa ajili ya kuzisaidia nchi zinazoendelea ambazo zinakabiliwa na chembembe zinazoathiri tabaka la Ozoni, imetenga kiasi cha dola za Marekani milioni 380 kuisaidiaChinaili kuondosha mazalia ya bidhaa za viwandani zinazotishia tabaka la Ozoni nchini humo .Masalia hayo ambayo yanaunda chembechembe zinazojulikana kitaalamu HCFCs, yanaweza kuondosha tabaka la Ozoni [...]

23/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Nchi isipolipa deni inaweka rehani vizazi vijavyo: UNCTAD

Kusikiliza / Supachai Panitchpakdi,Katibu Mkuu UNCTAD

Baraza la kijamii na kiuchumi la Umoja wa Mataifa ECOSOC leo limekuwa na mjadala kuhusu deni la nje ambapo washiriki wameangalia yale waliyojifunza kutokana na nchi kupata mikopo ya kigeni, athari zake na mchakato wa kufanya mikopo ya kigeni kuwa na manufaa zaidi kwa nchi husika na dunia kwa ujumla. Akitoa hotuba katika mkutano huo, [...]

23/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Madhara ya tetemeko la ardhi Uchina yabainika zaidi: OCHA

Kusikiliza / Shirika la OCHA

Yapata watu mia mbili wamekufa na wengine zaidi ya elfu kumi na mbili wamejeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi  lenye uharibifu mkubwa lililolikumba eneo la Lushan katika jimbo laSichuannchiniChinaApril 20. Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kratibu wa Misaada ya Kibinadamu, OCHA, wakati vifo na majeruhi hao wakiripotiwa maeneo mengi hayafikiki na takwimu hizo [...]

23/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waendesha mafunzo kwa maafisa wa serikali ya Somalia

Kusikiliza / somalia-map1

Kundi la wataalamu ambao walikwenda ughaibuni na hatimaye kurejea nyumbani Somalia limemaliza awamu yake ya kwanza ya utoaji mafunzo kwa maafisa wa serikali. Kundi hilo lenye wataalamu saba, lilirejea mjini Mogadishu na kuanzisha mafunzo yanayofahamika kama mafunzo kwa wakufunzi linaendesha kampeni ya kuwajengea uwezo maafisa wa serikali Mafunzo hayo ya siku mbili yameratibiwa kwa ushirikiano [...]

23/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IOM lawasafirisha raia wa Sudan Kusini wanaarudi nyumbani

Kusikiliza / Watu wa Sudan Kusini wasafirishwa makwao

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linaendelea na huduma ya kuwasafirisha kwa njia ya ndege zaidi ya raia 700 wa Sudan Kusini ambao wamekuwa wakisubiri kusafirishwa kwenda kwa jimbo laUpper Nilenchini  Sudan Kusini. Joseph Msami na taarifa kamiliWatu hao ni sehemu ya kundi la watu 1,030 waliosafirishwa na kanisa la Inland Church kutoka mji mkuu [...]

23/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali mbaya ya usalama yatatiza huduma muhimu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / Hali tete ya usalama yakatiza shughuli CAR

Hali ya usalama kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati inasalia tete ikitatiza jitihada za utoaji wa chakula na mashirika ya kutoa misaada kwenye maeneo yaliayoathiriwa na mizozo nchini humo kwa mujibu wa Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA.Mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa yamepunguza au kufutilia mbali shughuli zao hususan [...]

23/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban arejelea wito wa kusimamishwa mapigano Syria

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na mwenzake wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu Arab League Nabil Elaraby,ambao kwa pamoja wamejadilia haja ya kupatikana suluhu juu ya mgogoro wa Syria. Viongozi hao pamoja na mjumbe maalumu kwenye mzozo huo Lakhdar Brahimi wamejadilia haja ya kuzileta pande zote kwenye meza ya majadiliano Katika [...]

23/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Msumbiji yatoa chanjo mpya ya watoto dhidi ya numonia

Kusikiliza / Serkali ya Msumbiji imeanza kuwapa watoto chanjo PCV10

Nchini Msumbiji hatma ya afya ya watoto dhidi ya magonjwa ya njia ya hewa hususan numonia imeanza kupata mwanga baada ya serikali ya nchi hiyo kuanza kuwapatia watoto chanjo mpya aina ya PCV10.Chanjo hiyo imeanza kutolewa kwa ufadhili wa mashirika mbali mbali ikiwemo ya Umoja wa Mataifa ya UNICEF, WHO na lile la ubia wa [...]

23/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031