Nyumbani » 22/04/2013 Entries posted on “Aprili 22nd, 2013”

Utoaji wa silaha kwa pande zinazozozana Syria ukomeshwe: Ban

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Matiafa, Ban Ki-moon, amesema utoaji wa silaha kwa pande zinazozozana nchini Syria wafaa ukomeshwe, akiongeza kuwa silaha zaidi zinamaanisha vifo zaidi, na uharibifu zaidi. Bwana Ban amesema hayo katika taarifa ilotolewa mara tu baada ya mkutano wake na Sheikh Hamad bin Jassim bin Jabr Al-Thani, Waziri Mkuu ambaye pia [...]

22/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usafi India: Bila Choo, Hupati Bi Harusi

Kusikiliza / usafi wa vyoo India

Takriban nusu ya idadi ya watu bilioni 1.2 nchini India, hawana vyoo. Kuna watu wengi zaidi walio na simu za mkononi kuliko vyoo. Kati ya kila vifo kumi, kimoja kinatokana na ukosefu wa usafi unaofaa. Kwa karne nyingi, imekuwa ni jambo la kawaida watu kwenda choo hadharani. Lakini sasa, serikali ya India imeanzisha mkakati wa, [...]

22/04/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Heko wananchi wa Iraq kwa kupiga kura: Ban

Kusikiliza / Moja ya eneo la kupigia kura

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amepongeza kitendo cha wananchi wa Iraq kupiga kura katika uchaguzi wa viongozi wa majimbo mwishoni mwa wiki.  Bwana Ban amesema kwa kutekeleza haki yao ya kikatiba, wananchi waIraq wamedhihirisha azma yao ya kutakuwa kuwa na nchi ya kidemokrasia.  Amesifu ari waliyokuwa nayo ya kupiga kura licha ya [...]

22/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban ashtushwa na ghasia na mauaji Borno Nigeria:

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameshtushwa na kushangazwa na ripoti za idadi kubwa ya vifo vya raia na uharibifu wa nyumba uliosababishwa na mapigano baina ya majeshi na makundi yenye itikadi kali kwenye mji wa Kaskazini wa Baga jimbo la Borno nchini Nigeria. Machafuko hayo yalitokea April 19 na Aprili 20 mwaka [...]

22/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Timu ya wataalamu wa UM yahitimisha tathimini ya kinu cha nyuklia cha Japan

Kusikiliza / Wataalamu wa UM wamehitimisha tathmini ya kinu cha Nuclear, Japan

Licha ya mafanikio kadhaa Japan inaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa na ngumu wakati huu ikijitahidi kufunga kinu chache cha nyuklia kilichoathirika vibaya na tetemeko la ardhi na Tsunami Machi 2011.Tamko hilo limetolewa na wataalamu kutoka shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA ambao Jumatatu wamehitimisha tathimini ya awali ya juhudi za kukifunga kinu chake [...]

22/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Balozi Mahiga alaani mauaji ya mwandishi wa habari Somalia

Kusikiliza / Balozi mahiga alaani mauaji ya mwanahabari Somalia

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa kwa ajili ya Somalia Balozi Augustine Mahiga amestushwa na kuhuzunishwa na tukio la jana jioni la kupigwa risasi na kuuawa kwa mwandishi wa habari Ibrahim Rageh, aliyekuwa akifanya kazi na Radio yaMogadishuna Televisheni ya Taifa.Balozi Mahiga amelaani kitendo hicho na kutaka watekelezaji wa mashambulizi hayo ya [...]

22/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jitihada ziongezwe kudhibiti vitisho vya matumizi ya nyuklia: UM

Kusikiliza / Mjadala kuhusu matumizi ya nyuklia

Huko Geneva, Uswisi siku ya kwanza ya kikao cha maandalizi ya mkutano wa nchi wanachama wa mkataba wa kudhibiti kuenea kwa matumizi ya nyuklia ilitawaliwa na mjadala kuhusu vitisho vya nyuklia vinavyofanywa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea na mpango wa nyuklia wa Iran kama anavyoripoti Jaison Nyakundi.(PKG YA JASON NYAKUNDI) Jumuiya ya [...]

22/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ahuzunishwa na hasara iliyosababishwa na tetemeko la ardhi nchini China.

Kusikiliza / Ban ahuzunishwa na tetemeko la ardhi, China

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea kuhuzunishwa kwake kutokana na vifo , majehara na uharibifu uliosababishwa na tetemeko la ardhi lililolikumba jimbo la Sichuan nchini China mwishoni mwa juma akisema kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa msaada unaohitajika.Kulingana na vyombo vya habari tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa 6.6 hadi 7 [...]

22/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lapata ripoti kuhusu hali ya Sahara Magharibi

Kusikiliza / Hali ya usalama si mbaya sana Sahara magharibi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limefanya mashauriano kuhusu Sahara Magharibi ambapo limepatiwa ripoti kuhusu hali ilivyo kwenye eneo hilo.Ripoti hiyo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pamoja na mambo mengine imeeleza kuwa hali ya usalama si mbaya sana na kumekuwepo na maandamano ya hapa na pale ya wananchi wakitoa madai mbali [...]

22/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kila mtu alinde sayari dunia kwa mustakhbali wa wote: UM

Kusikiliza / Kila mtu alinde sayari

Wakati mustkhbali wa dunia uko hatarini kutokana na vitendo vinavyohatarisha uwepo wa sayari hii, kila mkazi ametakiwa kuwa makini katika kuhifadhi na kulinda mazingira kwa kuwa hakuna pahala pengine pa kukimbilia na huo ni wito kwa siku ya kimataifa ya kulinda sayari dunia hii leo kama anavyoripoti Grace Kaneiya. (PCKG- Grace) Kauli hizo zimetolewa mjini New [...]

22/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Marekani yaipatia WFP ngano kwa ajili ya wakimbizi wa Syria

Kusikiliza / Marekani yatoa ngano kwa ajili ya watu wa Syria

Meli ya Marekani yenye shehena ya ngano  ya kutosheleza watu zaidi ya Milioni Moja kwa kipindi cha miezi minne imeshusha shehena hiyo kwa ajili ya mgao kwa raia wa Syria ikiwa ni sehemu ya msaada wa dharura wa chakula unaotolewa na Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP.  Ikiwa imebeba tani 25,000 za ngano yenye thamani [...]

22/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yalaani kubakwa kwa mtoto wa miaka mitano India

Kusikiliza / UNICEF lalaani kubakwa kwa mtoto India

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limelaani kitendo cha kubakwa kwa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitano hukoNew Delhi,India. Assumpta Massoi na maelezo zaidi. (Taarifa Assumpta) Katika taarifa yake, UNICEF imesema kitendo dhidi ya mtoto huyo ni dalili dhahiri kuwa hatua za pamoja na za dharura zahitajika ili kuhakikisha wasichana [...]

22/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tutumie siku ya leo kurejelea ahadi ya kulinda dunia: Ban

Kusikiliza / Sayari dunia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe wa siku ya kimataifa ya kuilinda sayari dunia hii leo na kusema kuwa siku hii ni fursa ya watu wote kurejelea wajibu wa pamoja wa kuishi bila kuharibu mazingira wakati huu ambapo sayari hii inakabiliwa na vitisho mbali mbali. Amevitaja vitisho hivyo kuwa ni pamoja [...]

22/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031