Nyumbani » 19/04/2013 Entries posted on “Aprili 19th, 2013”

Mkutano wa UN Habitat wahimitishwa

Kusikiliza / UN Habitat

Mkutano wa 24 ambao hufanyika kila baada ya miaka miwili unaohusisha uongozi wa Baraza la Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi , UN Habitat , umemalizika mjini Nairobi Kenya, kwa makubaliano juu ya ukuaji endelevu wa miji na umuhimu wa jukumu la shirika hilo kwa Umoja wa Mataifa. Mkutano huo wa siku tano pia [...]

19/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

“Elimu Kwanza”:Kuwekeza katika elimu kunalipa

Kusikiliza / Mtoto darasani

Ingawa hatua kubwa zimepigwa katika mwongo mmoja uliopita, nchi nyingi za kipato cha chini bado zimebaki nyuma katika harakati za kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia kuhusu elimu ifikapo mwaka 2015. Ungana basin a Joshua Mmali katika makala hii inayoanza kwa kumulika mikutano ambayo imefanyika mjini Washington Marekani, ikiangazia suala la elimu, na kile kinachotakiwa [...]

19/04/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake DRC waandamana kupinga kikosi cha waasi

Kusikiliza / Wanawake DRC

  Wiki hii nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo DRC Kumeshuhudiwa maandamano ya wanawake wakipaza sauti zao kwa jumuiya ya kimataifa hususani ni Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR juu ya hofu ya kufuatia uwepo wa kikosi cha waasi wa ukombozi Rwanda FDRL nchini mwao. Akina mama hao wanaharakati walikusanyika  eneo la Goma [...]

19/04/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Kila kizazi na kifo kihesabiwe:Wito kutoka Bangkok

Kusikiliza / ESCAP count

Mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu usajili wa umma na takwimu muhimu zinazohitajika umemalizika huko Bangkok Thailand ambapo serikali, mashirika ya Umoja wa Mataifa na yale ya maendeleo yametoa wito kwa nchi zote duniani kuhakikisha matukio muhimu kama uzazi na kifo pamoja na sababu za kifo yanasajiliwa. Washiriki wamesema hatua hiyo ni muhimu kwani itawezesha [...]

19/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na mauaji ya mlinzi wa amani huko Darfur

Kusikiliza / UNAMID

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa serikali ya Sudan kuwasaka hadi kuwapata wahusika wa shambulio la leo asubuhi huko Darfur Mashariki lililosababisha kifo cha mlinda amani mmoja kutokaNigeriana kujeruhi wengine wawili. Msemaji wa Ban amemkariri Katibu Mkuu akilaani vikali shambulio hilo lililofanywa na watu wasiojulikana na ametuma rambirambi kwa familia na [...]

19/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Sasa naifahamu fika Syria, mpango wao ndio utakaokwamua nchi yao: Brahimi

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu katika mzozo wa Syria Lakhdar Brahimi amesema sasa anaifahamu fika nchi hiyo na kwamba suluhu ya mzozo wa Syria itokane na mpango wa wananchi wenyewe na siyo mpango wake yeye.  Brahimi amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjiniNew York, baada ya [...]

19/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nishati endelevu ni muhimu kwa maendeleo:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-Moon katika kikao cha nishati endelevu huko Washington DC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema nishati endelevu ni muhimu kwa karibu kila changamoto zinazokabili dunia ikiwamo kuwakwamua watu kutoka kwenye umaskini kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabia nchi, kuwezesha biashara, shule na kuboresah huduma za kliniki ili kuwawezesha wanawake. Akifungua mkutano wa bodi ya ushauri wa nishati endelevu mjiniWashington, Bwana [...]

19/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Suala la kurejeshwa makwao kwa Wakimbizi wa Rwanda laangaziwa

Kusikiliza / Wakimbizi wa Rwanda kurudi nyumbani kwa hiari

Mkutano wa mawaziri wa Afrika uliofanyika Pretoria wazungumzia hatma ya wakimbizi wa Rwanda kurejea makwao kwa hiari kama anavyoripoti Joseph Msami (TAARIFA YA MSAMI) Nchi kadhaa za Afrika zinazohifadhi idadi kubwa ya wakimbizi wa Rwanda pamoja na Rwanda, zimeelezea dhamira zao za kutatua tatizo la muda mrefu la wakimbizi wa Rwanda, kwa mujibu wa mkakati [...]

19/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wa Ethiopia Yemen wakabiliwa na hali ngumu: IOM

Kusikiliza / Wakimbizi waethipia walioko Yemen warudishwa makwao

Ujumbe wa mashirika ya kibinadamu, likiwemo Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, ukiongozwa na Mratibu wa shughuli za Umoja wa Mataifa nchiniYemen, Ismail Ould Cheikh Ahmed, jana Aprili 18 ulizuru mpaka kati ya Yemen na Saudia na kujionea mateso wanayokumbana nayo maelfu ya wahamiaji kutoka Pembe ya Afrika.Ziara hiyo imefuatia uvamizi wa hivi karibuni wa [...]

19/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kongamano la misitu lafikia ukingoni huko Istanbul

Kusikiliza / Mabunge wafanya majadiliano kuhusu misitu

Mazungumzo juu ya matokeo ya kongamano kuhusu misitu yanaendelea mjiniIstanbul huku vikao vikitarajiwa kuendelea baadaye leo.Mkurugenzi wa kongamano la misitu la Umoja wa Mataifa Jan McAlpine amewaambia waandishi wa habari kuwa kongamano hili limeweka msingi mpya katika usimamizi wa misitu. Anasema kuwa usimamizi mwema wa misitu unamaanisha usimamizi wa misitu na miti nje ya misitu [...]

19/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waitaka Iraq kusitisha unyongaji watu

Kusikiliza / Unyongaji watu usitishwe,UM

  Jumla ya watu 33 wamenyongwa nchini Iraq mwezi uliopita huku wengine 150 wakitarajiwa kunyongwa siku zinazokuja kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.Serikali ya Iraq inashikilia msimamo wake kuwa wanaonyongwa ni wale wanaohusuka kwenye vitendo vya kigaidi na uhalifu mwingine dhidi ya raia. Mkuu wa haki za binadamu kweneye [...]

19/04/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Tukishindwa kulinda mazingira, tumeshindwa kulinda haki za binadamu," waonya wataalamu wa UM

Kusikiliza / Ni lazima tulinde mazingira yetu, wataalamu, UM

Kundi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa wameonya kuwa, iwapo dunia itashindwa kulinda mazingira, basi itakuwa imeshindwa pia kulinda na kuzitetea haki za binadamu. Wakizungumza mjini Geneva kwenye kilele cha siku ya dunia, wataalamu hao wamesema kuwa kadri binadamu anavyoshindwa kuyatunza mazingira ndivyo anavyozalisha janga litakalomfanya ashindwe kufurahia haki za msingi za binadamu, Ikiwa [...]

19/04/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

UNHCR yataka fedha kuwahudumia wakimbizi wa Mali

Kusikiliza / UNHCR yahitaji ufadhili kwa ajili ya mahitaji ya wakimbizi, Mali

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limetoa wito wa kuongeza mafungu ya fedha kwa ajili ya kugharimia usambazaji wa mahitaji muhimu wa maelfu ya wakimbizi wa Mali na wale waliokosa makazi. Shirika hilo limesema kuwa linahitaji kiasi cha dola za Marekani milioni 144 kwa ajili ya kufanikisha mipango yake ya kuwahudumia wakimbizi [...]

19/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maelfu ya watoto nchini Mali hatarini kupata utapiamlo

Kusikiliza / Watoto waugua utapiamlo, Mali, UNICEF

Kiasi cha watoto 700,000 nchiniMaliwako hatarini kukubwa na matatizo ya utapiamlo, kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama katika eneo la kaskazini ambako makundi ya waasi yanaendesha harakati za kijeshi.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limesema kuwa hali ya utoaji wa huduma za kijamii kwenye shule pamoja na usambazaji wa maji [...]

19/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Askari wa kulinda amani auawa Darfur

Kusikiliza / Askari mlinda amani auawa

Taarifa ya Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur, UNAMID imetangaza kuuawa kwa askari mmoja wa kulinda amani asubuhi ya leo huko Muhajeria, Darfur Mashariki, huku wengine wawili wakijeruhiwa.UNAMID inachunguza tukio hilo lililotokea baada ya watu wasiojulikana kushambulia kundi la ujumbe huo kwenye eneo hilo. UNAMID inasema uchunguzi huo [...]

19/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNICEF yahofia watoto kukosa chanjo

Kusikiliza / Watoto wakipatiwa chanjo

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF lina wasiwasi kuwa matarajio ya watoto wote duniani kupata chanjo muhimu yanaweza kutumbukia nyongo kutokana na baadhi ya nchi kutotenga bajeti za kampeni hiyokamaanavyoripoti Joshua Mmali. (TAARIFA JOSHUA) UNICEF inaingia hofu hiyo kwa kuwa takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2011 watoto Milioni Moja na Nusu duniani wasingalifariki [...]

19/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikwazo vya kiurasimu huko Syria viondolewe: Baraza la Usalama

Kusikiliza / Kikao cha baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetaka vikwazo vyote vile vya kiurasimu vinavyokwamisha upelekaji wa misaada ya kibinadamu kwa wananchi wa Syria walionaswa katika mzozo wa kivita ndani ya nchi yao viondolewe.  Rais wa baraza hilo Balozi Eugène-Richard Gasana ametoa tamko hilo la baada ya kikao cha mashauriano kuhusu Syria ambapo maafisa waandamizi wa [...]

19/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930