Nyumbani » 18/04/2013 Entries posted on “Aprili 18th, 2013”

Suala la jinsia ni muhimu katika kuelewa ustawi wa miji:UNHABITAT

Kusikiliza / Habitat women youth

Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT linasema miji bora , inayojumuisha wote na yenye ustawi inapaswa kutambua mchango wa kila raia, yaani wanaume, wanawake na vijana. Hii ni muhimu wakati huu dunia ikikabiliwa na athari za mdororo wa kiuchumi na matatizo ya kifedha ambayo yamesababisha madhara mengi yakiwemo mabadiliko ya hali ya hewa, [...]

18/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuwaelimisha watoto sasa kutazaa matunda katika vizazi vijavyo: Ban

Kusikiliza / Wakati wa mkutano Washington DC

Wakati ulimwengu unakumbwa na uhaba wa fedha na rasilmali, viongozi wanatakiwa kuangazia elimu katika uwekezaji wa rasilmali hizo haba. Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo mjini Washington Marekani wakati wa mkutano wa kamati ya kwanza ya ngazi ya juu kuhusu mkakati wa kimataifa wa Elimu Kwanza, ambao ulizinduliwa [...]

18/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa CAR wakimbilia nchi ya DRC

Kusikiliza / Wakimbizi waelekea DRC

Huku kukiwa na taarifa za kuendelea kwa mapigano ndani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ,katika mji mkuu Bangui maelfu ya raia wa nchi hiyo wanakimbia ili kutafuta hifadhi na…………………. kwa sasa wamekuwa wakivuka mto uitwao Oubangui na kutafuta makazi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na katika jimbo la Orientale. Joseph Msami ameandaa taarifa ifuatayo.

18/04/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNHCR aonya hali mbaya Syria

Kusikiliza / Antonio Guterres

  Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Antonio Guterres, amelitahadharisha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba ikiwa mapigano hayataakomeshwa hima nchini Syria, nusu ya raia wa nchi hiyo yaani nilioni 20, watakuwa katika uhitaji mkubwa wa misaada ya kibindamu kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Akilihutubia baraza hilo [...]

18/04/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Taasisi za UM zaungana kuboresha hali ya udongo katika ardhi kame

Kusikiliza / Umuhimu wa kuhifadhi udongo

Taasisi mbili za Umoja wa Mataifa zimetiliana saini mradi wa kutumia teknolojia ya nyuklia kutathmini hali ya udongo katika ardhi kame, kama njia mojawapo ya kuepusha mmomonyoko wa ardhi.Shirika la nishati ya atomiki duniani, IAEA na taasisi ya Umoja wa Mataifa ya kusimamia mkataba wa kudhibiti na kuzuia kuenea kwa jangwa duniani, (UNCCD) wametia saini [...]

18/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Siku ya kimatiafa ya kuilinda dunia kuadhimishwa tarehe 22 mwezi huu

Kusikiliza / FAO itashiriki siku ya kimataifa ya kulinda dunia

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO liko kwenye mstari wa mbele katika maandalizi ya siku ya kimataifa ya kuilinda dunia ambayo itaadhimishwa tarehe 22 mwezi huu.Balozi mwema wa FAO Khaled ambaye ni mwanamuziki maarufu kutoka Algeria, atatumbuiza siku hiyo akishirikina na mwanamuziki kutoka Italia Fiorella Mannoia mjini Milan. Jumatatu ijayo zaidi [...]

18/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kuwait yataoa ufadhili kwa mashirika yanayotoa huduma nchini Syria

Kusikiliza / Antonio Guteress,wakati wa kupokea ufadhili wa Kuwait kupitia Balozi

Serikali ya Kuwait imetoa dola milioni 275 kwa mashirika tisa ya Umoja wa Mataifa yanayotoa huduma za kibinadamu nchiniSyria.Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limepokea dola milioni 110, Shirika la mpango wa chakula duniani FAO dola milioni 40, la kuhudumia watoto UNICEF dola milioni 53 huku Shirika la afya duniani WHO nalo [...]

18/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watoto wengi wanaendelea kuuliwa CAR-UNICEF

Kusikiliza / Kuna ongezeko la vifo vya watoto, CAR

Kumekuwa na ongezeko la vifo vya watoto wanaouwawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ikiwemo wale wanaouwawa wakati wakiwa kwenye maeneo ya kucheza na wengine kanisani.Aidha ripoti iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF imesema pia makundi mengine ya watoto wamejeruhiwa kufuatia kuongezeka kwa vitendo vya ghasia na unyanyasaji kwa watoto. [...]

18/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kampeni kubwa ya chanjo ya Polio na Surua yaanza Jordan

Kusikiliza / Kampeni ya chanjo ya polio na surua,Jordan

NchiniJordankampeni kubwa ya chanjo dhidi ya magonjwa ya Polio na surua imeanza katika kambi ya wakimbizi ya Za'atari wakati huu wa hofu ya mlipuko wa magonjwa hayo kutokana na mrundikano mkubwa wa watu. Kampeni hiyo inaendeshwa kwa pamoja na serikali yaJordanna mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiwemo la afya, la wakimbizi na lile la watoto. [...]

18/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya Syria ni janga la kibinadamu: OCHA

Kusikiliza / Valerie Amos, Mkuu wa OCHA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limejulishwa vile ambavyo wafanyakazi wa misaada wanakumbwa na vikwazo wanaposambaza misaada ya kibinadamu wananchi wa Syria walionaswa kwenye mgogoro wa kivita ambao shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA limeutia ni janga la kibinadamu. Taarifa hiyo imewasilishwa na Mkuu wa OCHA Valerie Amos [...]

18/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano kuhusu usajili wa umma na takwimu muhimu waanza mjini Bangkok

Kusikiliza / Mkutano wa usajili wa umma na takwimu muhimu waanza, Bangkok

Mkutano wa siku mbili kuhusu usajili wa watu na takwimu muhimu zinazohitajika kuzingatiwa katika mipango ya maendeleo, umeanza leo mjini Bangkok, Thailand. Joseph Msami ana maelezo zaidi kuhusu mkutano huo   (TAARIFA YA JOSEPH MSAMI)   Mkutano huo wa kimataifa umaeandaliwa na Shirika la Afya Duniani, (WHO) na Mtandao wa Takwimu za Afya (HMN), kwa [...]

18/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID yaomba Sudan iwezesha misaada kufikia raia

Kusikiliza / Jaribio barabarani eneo la kaskazini na magharibi mwa Darfur

Mkuu wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika nchini Sudan, UNAMID, Mohammed Ibn Chambas amekuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya ndani wa Sudan. Ibrahim Hamid mjini Khartoum.Katika mazugumzo hayo ameiomba serikali ya Sudan kusaidia UNAMID na misafara ya magari ya misaada kuwafikia raia waliotafuta hifadhi huko Muhajeria na [...]

18/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ubinafsishaji sekta ya Kahawa Burundi usubiri kwanza: Mtaalamu

Kusikiliza / Sekta ya kahawa isibinafsishwe, Burundi

  Wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya chakula na deni la nje wametaka kusitishwa kwa utekelezaji wa sera za ubinafsishaji wa sekta ya kahawa nchini Burundi zinazoongozwa na Benki ya dunia hadi pale tathmini ya madhara yake kwa haki za binadamu utakapofanyika. Grace Kaneiya na maelezo zaidi.(RIPOTI YA GRACE) Mapato yatokanayo na [...]

18/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usimamizi wa Haki za binadamu katika sekta ya biashara Marekani kumulikwa

Kusikiliza / Haki za binadamu biasharani kumulikwa, Marekani

  Jopo la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu biashara na haki za binadamu litakuwa na ziara ya siku 10 nchini Marekani, lengo ni kuangalia iwapo sekta ya biashara nchini humo inazingatia mwongozo wa biashara na haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. Mmoja wa wataalamu hao Michael Addo amesema ziara hiyo ni mwaliko [...]

18/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mawaziri wa Fedha wakutana Washington, Marekani

Kusikiliza / Mawaziri wa fedha wakutana DC

Mawaziri wa fedha na viongozi wengine kutoka kote duniani wanakutana mjini Washington, DC Marekani katika mkutano wa kila mwaka unaoandaliwa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, IMF. Miongoni mwa wale wanaohudhuria mkutano huo ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ambaye amesema anataraji mkusanyiko huo wa viongozi wa ngazi ya [...]

18/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930