Nyumbani » 17/04/2013 Entries posted on “Aprili 17th, 2013”

Mamilioni ya watoto duniani wakosa chanjo muhimu: WHO

Kusikiliza / Mtoto akipatiwa chanjo

Ikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa maadhimisho ya wiki ya utoaji chanjo duniani tarehe 20 mwezi huu, Shirika la afya duniani, WHO limesema takribani watoto Milioni 22 hususan katika nchi zinazoendelea hawajapatiwa chanjo za msingi za kuwakinga dhidi ya magonjwa hatari. WHO inasema mifumo dhaifu ya utoaji wa huduma za afya pamoja na migogoro [...]

17/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vongozi kujadili tatizo la elimu duniani

Kusikiliza / Shule DRC

  Ikiwa zimebaki siku zisizozidi 1000 kufikia tarehe ilowekwa kutimiza Malengo ya Maendeleo ya Milenia mwaka 2015, viongozi mbalimbali wakiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, Rais wa Bank ya Dunia Jim Yong Kim pamoja na Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya elimu kimataifa Godon Brown, wataongoza mjadala kuhusu [...]

17/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hali ya usalama yarejea Mogadishu: Mahiga

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UM nchini Somali, Balozi Augustine Mahiga

Hali ya usalama imeripotiwa kurejea mjiniMogadishu, nchiniSomalia, siku tatu baada ya mashambulizi ya kushtukiza mjini humo yaliyosababisha vifo vya makumi kadhaa ya watu na wengine kujeruhiwa. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Balozi Augustine Mahiga ambaye katika mahojiano maalum na Grece Kaneiya wa Idhaa [...]

17/04/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Sera lazima zishughulikie hatari za zamani za masuala ya fedha ili kukabili changamoto mpya:IMF

imf-logo_high

Shirika la fedha duniani IMF linasema mfumo wa kimataifa wa fedha imeimarika kuliko ilivyokuwa miezi sita iliyopita, lakini bado kuna changamoto kadhaa. Ripoti mpya ya IMF kuhusu hali ya kifedha duniani inasema watunga sera wasipochukua hatua za kushughulikia matatizo ya awali, mafanikio yaliyopatikana katika masoko ya fedha hayatoendelea na changamoto mpya zitajitokeza. Ripoti hiyo inaangazia [...]

17/04/2013 | Jamii: Taarifa za dharura | Kusoma Zaidi »

Umaskini umepungua duniani lakini bado kuna changamoto kubwa: Benki ya Dunia

Kusikiliza / Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim

Ripoti ya Benki ya Dunia imesema kuwa idadi ya watu wanaoishi kwa chini ya dola moja na robo kila siku imepungua kwa kiwango kikubwa katika miongo mitatu iliyopita kutoka nusu ya idadi nzima ya watu duniani mwaka 1981, hadi asilimia 21 tu mwaka 2010, licha ya idadi ya watu maskini kupanda kwa asilimia 59 katika [...]

17/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mali, DRC, CAR, na Syria kwenye ajenda ya mkutano wa Ban na waandishi wa habari

Kusikiliza / Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amekutana na waandishi wa habari mjini New York na kuzungumza kuhusu masuala mseto yanayohusu amani na usalama.Miongoni mwa nchi alizoangazia katika mkutano huo, ni Mali, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Syria na Jamhuri ya Watu wa Korea Kaskazini, DPRK. Kuhusu Syria, Bwana Ban amesema baa la vita [...]

17/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mwandishi aliyeko gerezani ashinda tuzo ya Uhuru wa vyombo vya habari

Kusikiliza / Mwanahabari wa Kiethiopia,  Reeyot Alemu atuzwa

Mwanahabari wa Ethiopia anayetumikia kifungo nchini humo Reeyot Alemu ameshinda tuzo la uhuru wa vyombo vya habari duniani la shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO kwa mwaka huu wa 2013, inayoitwa UNESCO Guillermo Cano. Mwandishi huyo wa habari mwanamke, alipitishwa na jopo huru la majaji wataalamu katika fani hiyo kwa [...]

17/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM walaani kuuawa kwa watoa misaada Syria

Kusikiliza / Valerie Amos

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mratibu wa misaada ya dharura Valerie Amos ametoa rambi rambi kufuatia mfululizo wa vifo vya wafanyakazi wa mashirika ya misaada nchini Syria ambapo mfanyakazi mwingine wa Chama cha halali nyekundu Uarabuni (SARC) Yousef Lattouf ameuwawa. Bwana Yousef Lattouf anakuwa mfanyakazi wa kumi na nane kuuawa katika [...]

17/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuimarika kwa miundo mbinu mijini kutaboresha uchumi na mazingira UNEP

Kusikiliza / Achim Steiner

Kuwekeza katika  miundombinu iliyo bora na teknolojia za kisasa vitatoa fursa nzuri ya kuwepo ukuaji wa uchumi mijini bila ya kuathiri mazingira, na hiyo ni  kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu miji katika nchi zinazoedelea.Inakadiriwa kuwa idadi ya watu wanaoishi mijini  itaongezeka kwa asilimia 70 ifikapo mwaka 2050. Ripoti hiyo inapendekeza kupunguza [...]

17/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lamulika ukatili dhidi ya wanawake katika vita

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limefanya kikao maalum kuangazia suala la ukatili wa kingono dhidi ya wanawake katika mazingira ya vita, kikao ambacho kilianza kwa kutoa heshima kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Margaret Thatcher na wahanga wa mabomu wakati wa mbio za Boston Marathon. Joshua Mmali na taarifa kamili. (Taarifa ya [...]

17/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu maalum wa UM kuhusu ukatili dhidi ya wanawake atazuru India

Kusikiliza / Rashida Manjoo

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake Rashida Manjoo atakuwa na ziara ya zaidi ya wiki moja nchini India kuanzia wiki ijayo, kubwa zaidi ni kutathmini vitendo dhalili dhidi ya wanawake nchini humokamaanavyoripoti George Njogopa.(TAARIFA YA GEORGE) Kwa mujibu wa Bi Manjoo unyanyasaji wa kijinsia unaendelea kusalia ,moja ya tatizo kubwa [...]

17/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID yataka misaada ya kibinadamu kwa raia huko Labado

Kusikiliza / Walinda amani kikosi cha UNAMID

Na sasa nchini Sudan ambako, baada ya vikosi vya Sudan Armed Forces kuutwaa mji wa mji wa Labado huko Darfur Mashariki, raia wanahitaji misaada ya kibinadamu kama anavyosimulia Grace Kaneiya. (Taarifa ya Kaneiya) Baada ya mji huo wa Labado kutwaliwa jana kufuatia makali yaliyozuka kwenye eneo hilo yaliyosababisha vifo vya raia wanne na wengine sita [...]

17/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mauzo ya bidhaa kimataifa yalishuhudia mkwamo mwaka 2012: UNCTAD

Kusikiliza / Mauzo ya bidhaa kimataifa yamekwama

Biashara ya bidhaa zinazouzwa nje ilishuhudia mkwamo mnamo mwaka 2012 baada ya kuongezeka kwa kiasi kikubwa miaka ya 2010 na 2011, kulingana na takwimu za Kamati ya Biashara na Maendeleo katika Umoja wa Mataifa, UNCTAD.Katika nchi zinazoendelea, mauzo ya nje yalipanda kwa asilimia 3.6, ingawa ongezeko hilo lilishuhudiwa katika nchi zinazouza bidhaa za mafutana gesi [...]

17/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Somalia ihakikishe usalama wa watendaji wa mahakama: Mtaalamu huru

Kusikiliza / Shamsul Bari

Serikali ya Somalia na Jumuiya ya kimataifa zimetakiwa kutokatishwa tamaa na mashambulio ya Jumapili na badala yake ziimarishe usalama kwa watendaji wa mahakama ili haki iweze kutendeka, hilo ni tamko la mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kama anavyoelezea Assumpta Massoi. (Taarifa Assumpta) Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya haki za binadamu [...]

17/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930