Nyumbani » 16/04/2013 Entries posted on “Aprili 16th, 2013”

Mahitaji yameongezeka nchini Chad:IOM

Kusikiliza / IOM-Logo

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM limesema idadi kubwa ya wahamiaji na wakimbizi wanaomiminika nchini Chad wamesababisha ongezeko la mahitaji ya kibinadamu ambayo nchi hiyo hiyo pekee haiwezi kutosheleza, na hivyo kuomba ufadhili wa haraka ili kuwanusuru. Katika mahojianao na Grace Kaneiya mseaji wa IOM Jumbe Omari jumbe anasema dola milioni tatu na nusu zinahitajika [...]

16/04/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Suluhu ya migogoro barani Afrika kumulikwa ndani ya Baraza Kuu la UM: Jeremic

Kusikiliza / Vuk Jeremić, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Vuk Jeremić amezungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani na kutangaza kuwa suala la usuluhishi wa migogoro barani Afrika kwa njia ya amani litamulikwa wakati wa mjadala wa wazi wa barazahilobaadaye mwezi huu. Bwana Jeremić amesema mfumo huo wa kuwa na mada maalum umekuwa wa mafanikio ambapo washiriki [...]

16/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WFP yajitahidi kufikisha msaada wa chakula kaskazini mwa Mali hali inavyozidi kuzorota

Kusikiliza / Hali ikizorota, WFP badi inafikisha msaada Mali

Shirika la mpango wa chakula, WFP, linafanya harakati za dharura likishirikiana na wadau wengine ili kuzifikia familia za watu ambao hawana chakula kwa sababu ya mzozo unaoendelea, hali ambayo intarajiwa kuzorota hata zaidi katika msimu unaoanza mwezi Aprili hadi Juni.Kufuatia ziara yake mjini Timbuktu wiki ilopita, Mkurugenzi wa WFP nchini Mali, Sally Haydock amesema hali [...]

16/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Adha za wakimbizi wa Syria zamulikwa

Kusikiliza / UM na mashirika wataka wakimbizi Syria isaidiwe

Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, jana kwa pamoja wamezipazia sauti pande zote katika mzozo wa Syria na serikali zenye ushawishi zifanye kila ziwezalo kuwaokoa watu wa Syria kutokana na watu wa Syria na ukanda mzima kutokana na baa la vita. Licha ya kuanisha msaada badounahitajika lakini wamesisitiza pande zinazozozana kuyaacaha mapigano hima. Ungana [...]

16/04/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Utafiti wabaini tishio la uhalifu wa kimataifa Afrika Mashariki na Pasifiki

Kusikiliza / Nembo ya UNODC

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia madawa ya kulevya na uhalifu UNODC leo inazindua tathmini ya tishio la uhalifu wa kimataifa wa kupangwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Pasifiki. Ripoti hiyo inaangalia jinsi uhalifu huo umesababisha masoko haramu kukua sambamba na yale halali, na yanakadiriwa kuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 90. [...]

16/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Majeshi ya Sudan yadhibiti mji wa Labado:UNAMID

Kusikiliza / Kikosi cha walinda amani, UNAMID

Vikosi vya pamoja vya Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika vya kulinda amani Darfur UNAMID vimesema vimepokea taarifa Jumanne asubuhi kwamba majeshi ya Sudan yanayoungwa mkono na Popular Defense Forces na kundi lingine lenye silaha yamechukua udhibiti wa mji wa Labado katika jimbo la Darfur Mashariki.Vikosi hivyo vilichukua usukani kutoka kundi la Sudan Liberation [...]

16/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa pande tatu kuhusu UNAMID waangazia usalama Darfur

Kusikiliza / Walinda amani wa UNAMID

      Hofu kuhusu ongezeko la visa vya kutokuwepo usalama na uwezo wa walinda amani wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa, Darfur (UNAMID) kuyafikia maeneo yaloathiriwa zaidi na mzozo yamefanywa masuala ya kipaumbele katika majadiliano ya kikao cha 15 cha mkutano wa mfumo wa pande tatu wa kuratibu shughuli za UNAMID. Kikao [...]

16/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya raia wa Sudan waliojikuta kwenye mapigano yatia wasi wasi.

Kusikiliza / Wakimbizi huko Darfur

  Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Ali Al-Za'tari amelezea wasiwasi uliopo kutokana na usalama wa raia walionaswa kwenye mapigano kati ya vikosi vya serikali na kundi la Sudan Liberation Army, Mashariki mwa Jimbo la Darfur. Umoja wa Mataifa unasema kuwa watu 36,000  wamepiga kambi karibu na makao ya  ujumbe wa pamoja wa Umoja [...]

16/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yalaani mashambulizi nchini Somalia

Kusikiliza / Ofisi ya Haki za binadamu ya UM

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani mashambulizi yaliyofanyika tarehe 14 mwezi huu dhidi ya msafara wa misaada karibu na uwanja wa ndege mjini Mogadishu pamoja na mahakama ya mkoa ya Banadir mjini humo ambapo raia 50 waliuawa  wakiwemo watu 35 waliokuwepo mahakamani. Mawakili watatu wakiwemo watetezi wawili maarufu wa haki za [...]

16/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mahakama za kusafirishwa zaanzishwa kwenye kambi ya wakimbizi Uganda: UNHCR

Kusikiliza / Mfumo wa mahakama za kusafirishwa umeanza, Uganda

Nchini Uganda, mfumo wa mahakama za kusafirishwa umeanza kujaribiwa mnamo Jumatatu Aprili 15 ili kurahisisha uwepo wa haki kwa wakimbizi ambao wamekosewa.Mradi huo unaoendeshwa kwenye kambi ya Nakivale kusini magharibi mwa nchi, umeanziswha na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR kwa ushirikiano na serikali yaUganda. Unatarajiwa kuwahudumia takriban wakimbizi 68,000 na raia wa Uganda 35,000 kwa [...]

16/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yaomba msaada wa kuwasadia wahamiaji na wakimbizi wanaongia nchini Chad

Kusikiliza / IOM linatoa ombi ili kusaidia wakimbizi wa Chad

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linatoa ombi wa kuwepo ufadhili zaidi  ili kuliwezesha kutoa misaada ya kibinadamu ya kuokoa maisha kwa maelfu ya wahamiaji wanaorejea nyumbani  na kuingia nchini Chad  kutoka sehemu nne za mpaka wa nchi hiyo.Karibu wahamiaji 17,000  raia wa Chad wameingia nchini mwao kwa muda wa majuma matatu yaliyopita kutoka eneo [...]

16/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Homa ya ndege yaendelea kusambaa China

Kusikiliza / Homa ya H7N9 inaendelea kusambaa China

Homa ya ndege aina ya H7N9 inaendelea kusambaa nchiniChina, huku vifo vikiongezeka, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO. (TAARIFA YA KANEIYA) Idadi ya watu ambao wameaga dunia kutokana na ugonjwa wa homa ya ndege nchini China inazidi kupanda na hadi sasa imefikia vifo 14 kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO. Nao watu [...]

16/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lapokea taarifa kuhusu hali halisi Cote d'Ivoire

Kusikiliza / Edmond Mulet

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepokea ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja huo kuhusu hali halisi ya usalama na amani huko Cote D'Ivoire.Ripoti hiyo iliyowasilishwa na Edmond Mulet, Msaidizi wa Katibu Mkuu katika operesheni za ulinzi wa amani. Ripoti hiyo pamoja na kueleza hali ya usalama kuwa bado si shwari sana, imeibuka [...]

16/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yaanza kuwasaidia waathirika wa mafuriko Msumbiji

Kusikiliza / Ramana ya Msumbiji

Shirika la Kimataifa la uhamiaji IOM limeanza kuzifanyia ukarabati nyumba zilizoharibiwa na mafuriko yaliyoyakumba maeneo mbalimbali nchini Msumbiji katika kipindi cha mwezi Januari mwaka huu. Kiasi cha familia 5,000 kilipoteza makazi yao kutokana na mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizojitokeza katika eneo la Kusin mwa bara la Afrika. Ama watu wengine 150,000 waliathiriwa na [...]

16/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WFP, TRC yaongeza usambazaji chakula kwa wasyria walioko Uturuki.

Kusikiliza / watoto nchini Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP likishirikiana na chama cha mwezi mwekundu cha Uturuki  limeongeza mpango wa usambazaji wa chakula kwa makambi ya wakimbizi nchini humo, kwa kuzifikia kambi nyingine nne ambazo zimefurika wakimbizi waSyriawanaokimbia machafuko nchini mwao.Hatua hiyo sasa inafanya jumla ya watu wanaopata msaada huko wa chakula nchini Uturuki [...]

16/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukiukwaji wa sheria Jamhuri ya Afrika ya Kati ukome: Pillay

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati

Hali ya sintofahamu inazidi kukumba Jamhuri ya Afrika ya Kati huku idadi ya watu waliouawa tangu waasi wapindue serikali ikiongezeka na raia wakikimbilia nchi jirani. Umoja wa Mataifa umetaka kukomeshwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamukamaanavyoarifu Assumpta Massoi.  (ASSUMPTA PKG )  Zaidi ya watu 119 wameuawa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu waasi wapindue serikali [...]

16/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031