Nyumbani » 15/04/2013 Entries posted on “Aprili 15th, 2013”

Umoja wa Mataifa wayakumbuka mauaji ya kimbari Rwanda

Kusikiliza / Vuk Jeremic

  Rais wa Baraza Kuu, Vuk Jeremic, amesema katika miaka baada ya mauaji ya kimbari, Wahutu na Watutsi nchini Rwanda wameweza kuja pamoja na ari mpya, ili kujenga nyumba ya haki na maendeleo kwenye msingi wa umoja na maridhiano, chini ya uongozi wa rais Paul Kagame. Katika kipindi cha takriban siku mia moja, yapata watu [...]

15/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maendeleo yapatikana katika kuepusha ukuaji wa kudumaa miongoni mwa watoto

Kusikiliza / Nembo ya UNICEF

Ripoti mpya ya shirika la kuhudumia watoto duniani, UNICEF imeonyesha mafanikio katika harakati za kupunguza kudumaa miongoni mwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.Kudumaa kunakumba watoto Milioni 165 wenye umri huo na UNICEF inasema kuwa kuboresha lishe ndio suluhu pekee kama anavyoarifu George Njogopa. (TAARIFA YA GEORGE) Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Anthony [...]

15/04/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mashambulizi ya bomu Boston

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

   Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani vikali mashambulizi ya bomu yalotekelezwa leo siku ya Jumanne mjini Boston, Marekani wakati wa mashindano ya kimataifa ya mbio za masafa marefu, maarufu kama Boston Marathon. Mashambulizi hayo yameripotiwa kuwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine kadhaa. Akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kumbukumbu ya [...]

15/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mashambulizi ya bomu Mogadishu

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amelaani vikali mashambulizi yalotekelezwa mjini Mogadishu mnamo tarehe 14 karibu na jumba la mahakama ya kikanda na jingine karibu na uwanja wa ndege, ambayo yanaripotiwa kuwaua watu. Bwana Ban ameyataja mashambulizi hayo kama vitendo vya kigaidi dhidi ya serikali, taasisi na watu wa Somalia. Ametum risala [...]

15/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yapazia sauti watu wa Syria wasaidiwe

Kusikiliza / baridi kali

Wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, leo kwa pamoja wamezipazia sauti pande zote katika mzozo wa Syria na serikali zenye ushawishi zifanye kila ziwezalo kuwaokoa watu wa Syria kutokana na watu wa Syria na ukanda mzima kutokana na baa la vita. Wakuu hao, Valerie Amos wa OCHA, Ertharin Cousin wa WFP, Antonio Guterres wa [...]

15/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tubadili mwelekeo wa kushughulikia migogoro: Rwanda

Kusikiliza / mushikiwabo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo amezungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani baada ya ufunguzi wa mjadala kuhusu uzuiaji wa migogoro barani Afrika na kusema wakati umefika Umoja wa Mataifa ubadili mwelekeo wa kushughulikia masuala hayo. Bi. Mushikiwabo ambaye nchi yake inashika kiti cha Urais wa Baraza la Usalama [...]

15/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni lazima tuboreshe maisha ya watu maskini: UN-Habitat

Kusikiliza / UNHABITAT council

Kikao cha 24 cha Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na nyumba na makazi (UN Habitat), kimeanza leo mjini Nairobi, huku viongozi wakitoa wito wa kuboresha maisha ya watu maskini duniani. Akifungua kikao hicho, rais mpya wa Kenya Uhuru Kenyatta, mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa yanatakiwa kutumia fursa ya kikao hicho cha wiki moja [...]

15/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashambulio mjini Mogadishu hayatukatishi tamaa: Balozi Mahiga

Kusikiliza / Kikosi cha AMISOM kikiwa kwenye doria mjini Mogadishu

  Siku ya Jumapili ilikuwa ya giza nene hukoMogadishu,Somalia baada ya kuwepo kwa mfululizo wa mashambulio ya mabomu wakati huu ambapo serikali ya nchi hiyo inaendelea kushirikiana na wadau mbali mbali kuimarisha usalama ili shughuli za maendeleo ziweze kufanyika. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Balozi Augustine Mahiga alizungumza na Joseph Msami [...]

15/04/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Biashara ya urembo yamwezesha mkimbizi kujitegemea

Kusikiliza / Rosette Wabenga

Mwanamke mmoja mkimbizizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ambae sasa anaishi Uganda ameweza kutimiza ndoto yake ya kujitegema kupitia biashara ya urembo. Mwanamke huyo Rosetta Wabenga ambae ni mama wa watoto watatu anasema kuwa amepitia mengi lakini sasa kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR anasema amepata mafanikio . [...]

15/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ufadhili wa misitu hauwezi kutegemea chanzo kimoja tuu:Benki ya Dunia

Kusikiliza / FOREST

Ufadhili wa sekta ya misitu lazima utoke katika vyanzo mbalimbali vikiwemo vya ndani na vya kimataifa , pamoja na sekta binafsi. Lakini tatizo la ufadhili wa sekta hiyo haliwezi kufumbuliwa kwa kutegemea chanzo kimoja. Hayo yamesemwa na Tuuka Castren mtaalamu na afisa wa wa masuala ya misitu, kilimo na maendeleo ya vijijini wa Benki ya [...]

15/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Serry azungumzia kujiuzulu kwa Fayyad

Kusikiliza / Robert Serry

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa katika mchakato wa amani Mashariki ya Kati Robert Serry leo amekutana na Waziri Mkuu wa Palestina aliyejiuzulu Salam Fayyad, kumshukuru kwa niaba ya Umoja wa Mataifa kutokana na mafanikio yaliyopatikana wakati wa uongozi wake. Bwana Serry amesema kiongozi huyo aliyejiuzulu sio tu kwamba amekuwa msuluhishi ambaye yeye anamheshimuwa kwa [...]

15/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lijikite katika kuzuia na si kutatua mizozo: Rwanda

Kusikiliza / Wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama

Baraza La usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala kuhusu jinsi ya kuzuia migogoro barani Afrika ambapo mwenyekiti wa mjadala huo alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda kama anavyo ripoti Joshua Mmali. (SAUTI YA JOSHUA) Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya kikao maalum kujadili suala la amani na usalama [...]

15/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu lafanya mjadala kuhusu udhibiti wa uchumi wa kimataifa

Kusikiliza / Baraza Kuu

Wakati harakati za kubuni vigezo vya ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 zikiendelea, mjadala umefanyika leo katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu udhibiti wa uchumi wa kimataifa.Wakati wa mjadala huo, rais wa Baraza Kuu, Vuk Jeremic, amesema kuwa kulingana na makubaliano ya Rio+20, sera zinazotungwa kwa ajili ya kuendeleza ukuaji wa kiuchumi [...]

15/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM wapongeza kuanza kwa upigaji kura Iraq kwa amani

Kusikiliza / Martin Kobler

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Martin Kobler ameelezea kuridhishwa kwake na kuanza kwa zoezi maalum la upigaji kura kuchagua magavana wa mabaraza nchini humo ambapo askari na polisi wamejitokeza kupiga kura kabla ya wananchi wengine kufanya hivyo wiki ijayo.Martin Kobler amesema hatua hiyo imefungua njia kuashiria kufanyika kwa uchaguzi [...]

15/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tanzania yajiandaa kupeleka askari DRC

Kusikiliza / Ujumbe kutoka Tanzania, Malawi na Afrika Kusini wawasili DRC

Harakati za maandalizi ya brigedi ya kusaidia ulinzi huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC zinaendelea ambapo nchi husika zinakamilisha shughuli hiyo miongoni mwao ni Tanzania kama anavyoripoti Assumpta Massoi.(Ripoti yaAssumpta) Takribani mwezi mmoja baada ya Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kuupatia ujumbe wake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, uwezo wa kuwa [...]

15/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhifadhi wa rasilimali za aina za mazao ni muhimu kwa maisha ya binadamu

Kusikiliza / Mahitaji ya lishe bora yanaongezeka

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kilimo na chakula duniani, FAO Dan Gustafson amewaeleza wajumbe wa tume ya uhifadhi wa aina mbali mbali za mazao duniani na kusema kadri idadi ya watu inavyoongezeka duniani na mahitaji ya lishe bora na ya kutosha inavyoongezeka ni lazima kuhifadhi rasilimali hizo kwa maisha ya binadamu. (Taarifa ya Kaneiya) [...]

15/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mahiga ashtushwa na mashambulizi Mogadishu

Kusikiliza / Augustine Mahiga

Mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Dkt. Augustine Mahiga ameelezea kushtushwa kwake na kulaani mashambulizi yaliyofanywa mjini Mogadishu nchini Somalia siku ya Jumapili na kusababisha vifo vya watu Kumi na Tisa huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongeza.   Balozi Mahiga ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa katika mahojiano maalum [...]

15/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031