Nyumbani » 12/04/2013 Entries posted on “Aprili 12th, 2013”

Wahamiaji wa Tawerika Libya wapata afueni kwa msaada wa IOM

Kusikiliza / Jumbe Omari Jumbe

Miaka miwili bada ya mapigano yalioikumba Libya, baadhi ya raia wa nchi hiyo, wamegeuka wahamiaji katika nchi yao kutokana na chuki za kisiasa. Mathalani jamii ya Tawerika yenye idadi ya takribani watu 30, 000 ambao wamesambaa sehemu kadhaa za mjini Tripoli na sehemu nyingine  kutafuta makazi. Kufuatia hilo Shirika la kimataifa la Uhamiaji IOM likishirikiana [...]

12/04/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban apongeza mazungumzo kati ya Bashir na Kiir

Kusikiliza / Rais Omar Al-Bashir wa Sudan na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameunga mkono mazungumzo yaliyofanyika hii leo huko Juba kati ya marais wa Sudan Omar Al Bashir na Salva Kiir wa Sudan Kusini na kusema anatiwa moyo na majadiliano hayo chanya yenye lengo la kuona makubaliano ya Addis Ababa ya mwezi Septemba mwaka jana yanafikiwa. Bwana Ban amewasihi [...]

12/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kila mtu ana fursa ya kuchochea kufikiwa kwa malengo ya Milenia: Ban

Kusikiliza / Malengo ya Maendeleo ya Milenia

Kampeni ya kuchochea utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia iliyoanza mapema wiki hii kwa kuhesabu siku Elfu moja zilizobakia kabla ya ukomo mwaka 2015, imetiwa shime hii leo hapa New York, Marekani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon alipozungumza na wawakilishi wa nchi wanachama na wafanyakazi wa Umoja huo. Bwana Ban amesema [...]

12/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhifadhi wa misitu kuchochea utalii Kenya: Kabugi

Kusikiliza / Msitu wa Mau nchini Kenya

Huko Istanbul, Uturuki mkutano wa kimataifa kuhusu mustakhbali wa misitu duniani unaendela na kubwa ni jinsi gani misitu inaweza kusaidia kuchochea maendeleo ya kiuchumi. Donn Bob wa Radio ya Umoja wa Mataifa aliyeko mjini humo aliratibu mahojiano na Hison Kabugi, Mkurugenzi wa Misitu na  Wanyamapori kutoka Kenya, mahojiano ambayo yaliendeshwa nami Joshua Mmali kutoka hapa [...]

12/04/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

IOM yatoa misaada kwa wakimbizi wa ndani Libya

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani Libya

  Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM kwa kushirikiana na asasi za kiraia 37 limeanza kugawa misaada isiyo ya chakula kwa raia walipoteza makazi katika makambi sehemu mbalimbali nchini Libya hususan katika mji wa Tripoli. Kwa mujibu wa msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe msaada huo unailenga jamii ya Tawerika yenye watu takriban 30,000 ambao [...]

12/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kumbukumbu ya Hammarskjöld yamulika usalama wa walinda amani

Kusikiliza / Askari walinda amani wa UNMIL

Ni wiki chache tu zimesalia hadi Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa, mnamo Mei 29. Kazi ya kulinda amani ni kazi inayohitaji ujasiri na kujitolea, kwani aghalabu kazi hii hufanyika katika maeneo na mazingira yasiyo salama. Mnamo siku ya Jumatano wiki hii, Umoja wa Mataifa ulifanya hafla maalumu ya kumkumbuka na [...]

12/04/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Twahitaji dola Milioni 19 kila wiki kuhudumia wakimbizi wa Syria: WFP

Kusikiliza / Wakati wa vitafunio, Syria

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limesema linaweza kulazimika kupunguza msaada wake kwa wakimbizi wa Syria iwapo halitapatiwa fedha zaidi.WFP imesema itahitaji dola Milioni 18 kwa miezi mitatu ijayo ili operesheni zake za usaidizi wa chakula hukoSyria na nchi jirani zinazohifadhi wakimbizi ziweze kuendelea hata baada ya mwezi Juni. Shirika hilo [...]

12/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WMO yaondoa jina la Sandy kwenye orodha ya vimbunga

Kusikiliza / WMO LOGO

Shirika la hali ya hewa duniani, WMO limeamua kuondoa rasmi jina Sandy katika orodha ya vimbunga vinavyopiga bahari ya Atlantiki. Uamuzi huo unafuatia kimbunga Sandy kusababisha madhara makubwa huko Jamaica, Cuba, Haiti na baadhi ya maeneo ya kati nchini Marekani, mwezi Oktoba mwaka jana. Msemaji wa WMO Claire Nullis akizungumza mjini Geneva, Uswisi amesema nafasi [...]

12/04/2013 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hatuwezi kuwa na ukuaji unaojali mazingira bila kuhifadhi bahari: FAO

Kusikiliza / Ni muhimu kuyajali mabahari

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, José Graziano da Silva, amesema leo ya kwamba, juhudi za kutokomeza njaa na kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi katika visiwa vya Pasifiki zitategemea ufanisi wa maendeleo endelevu, pamoja na matumizi yenye busara ya mabahari na uvuvi. George Njogopa ana maelezo zaidi(TAARIFA YA GEORGE) [...]

12/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali nchini Mali bado ni tete:UM

Kusikiliza / Wakimbizi Mali, hali ni tete

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema hali bado ni tete nchiniMalihuku watu wakiendelea kukimbia na maelfu wakihitaji msaada. Mashirika ya OCHA, WFP na UNHCR, yote yakijitahidi kwa kila njia kuokoa maisha ya mamilioni ya watukamaanavyoarifu Grace Kaneiya.(SAUTI YA KANEIYA) Mashirika hayo yanatumai kuwafikia mamilioni ya watu kwa msaada wa chakula wakiwemo wakimbizi wa ndani 270,000  [...]

12/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watu wanaoishi kwenye kambi za muda Haiti, yapungua:IOM

Kusikiliza / Ramani ya Haiti

Idadi ya watu waliohama makwao nchini Haiti na wanaoishi kwenye kambi inazidi kupungua.Makadirio ya hivi majuzi yanaonyesha kupungua kwa watu 27,230. Msemaji wa shirika la kimataifa la uhamiaji Jumbe Omari Jumbe amesema ikilinganishwa na watu milioni 1.5 waliohama makwao baada ya tetemeko la mwaka 2010 idadi ya wakimbizi wa ndani imepungua kwa asilimia 79. Lakini [...]

12/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watu 50,000 wahama makwao kutokana na mapigano kwenye jimbo la Darfur

Kusikiliza / Hali tete kupelekea wakimbizi kutoka Darfur kuelekea Chad

UNHCR inasema kuwa wakimbizi hao wanahitaji huduma za kibinadamu kwa kuwa hivi sasa wamepiga kambi kwenye eneo lililo umbali wa kilomita 200 kutoka kwa ofisi ya UNHCR.Melisa Fleming kutoka UNHCR anasema kuwa idadi ya wakimbizi inatarajiwa kuongezeka siku zinazokuja wakati mapigano yanapoendelea kuchacha. (SAUTI YA MELISSA) Tangu mwaka 2003 zaidi ya watu 300,000 wamevuka mpaka [...]

12/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Anga za juu ni pahala pa wote; wasichana wajifunze hesabu na Sayansi: Anousheh

Kusikiliza / Anouseh Ansari

Wakati leo ni siku ya kimataifa ya kuadhimisha siku ambayo chombo cha kwanza kikiwa na binadamu kilienda anga za juu, mmoja wa wahandisi wanawake nchini Iran ambaye amewahi kwenda anga za juu kutembea na kujifunza Bi. Anousheh Ansari amesema watoto wa kike wajifunze hesabu na sayansi zaidi ili waweze kufuata nyayo za mwanamke wa kwanza [...]

12/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto waendelea kutumiwa na vikundi vya wapiganaji CAR: UNICEF

Kusikiliza / Watoto waliokuwa wakitumiwa na vikundi vya wapiganaji

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuna taarifa kuwa watoto bado wanatumikishwa kwenye vikundi vya kijeshi, kitendo ambacho ni kinyume na haki za binadamukamaanavyoripoti Assumpta Massoi.  (SAUTI YA MASSOI) Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limesema lina ushahidi wa kutosha kuwa watoto kuendelea kutumiwa na vikundi vyenye silaha huko Jamhuri ya Afrika [...]

12/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031