Nyumbani » 09/04/2013 Entries posted on “Aprili 9th, 2013”

Taa za kutumia nishati ya jua kukabiliana na ubakaji Somalia

Kusikiliza / Wakimbizi katika moja ya kambi mjini Mogadishu

  Katika kupambana na ukatili wa kijinsia nchini Somalia, Shirika la kimataifa la masuala ya umeme la nchini Japan, Panasonic, kwa kushirikiana na shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM,  limeanzisha utafiti wa namna taa za kutumia nishati ya miale ya jua zinavyoweza kupunguza ukatili huo katika kambi za wakimbizi na wahamiaji . Mchango huo wa [...]

09/04/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban awa na mazungumzo na Pope Francis huko Vatican

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Pope Francis wa I

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekuwa na mazungumzo na kiongozi wa kanisa katoliki duniani Pole Francis wa kwanza huko Vatican, Italia ambapo amesema kiongozi huyo ana wamejadili jinsi ya kufanikisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia kwa kuhakikisha usimamizi wa haki miongoni mwa jamii. Bwana Ban amesema ilikuwa ni heshima kubwa kuwa na mazungumzo [...]

09/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mamlaka za makundi ya Seleka bado yanawaingiza watoto katika jeshi: Vogt

Kusikiliza / Margaret Vogt

Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Margaret Vogt, amesema kuwa uongozi wa kundi la Seleka lililonyakuwa mamlaka katika Jamhuri ya Afrika ya kati hauna utaratibu wa kisheria, na kuna ripoti za kundi hilo kuwashurutisha watoto kuingia katika jeshi. Baada ya kulihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Bi [...]

09/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaendelea kuubeba mzigo wa wakimbizi wa DRC Uganda

Kusikiliza / wakimbizi wa DRC

Umoja wa Mataifa unaendelea na juhudi za kuwasaidia wakimbizi wanaosababishwa na mapigano katika nchi mbalimbali, kama vile nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo hali inaripotiwa kuendelea kuwa tete na kusababisha maelfu ya raia kukimbilia nchi jirani kutafuta hifadhi. Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi hadi sasa takribani raia milioni 2 [...]

09/04/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Syria yaripotiwa kugomea uchunguzi, Ban azungumza

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Wakati maandalizi ya jopo tangulizi la kuchunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchini Syriayakiwa yamekamilika, imedaiwa kuwa serikali ya Syria haikubaliani na muundo na mfumo wa uchunguzi huo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambaye aliunda jopohilo, alipoulizwa na waandishi wa habari mjini Vatican kuhusu taarifa hizo amesema hajapata mawasiliano rasmi kutoka [...]

09/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laitaka serikali ya Sudan Kusini kuchunguza mauaji ya walinda amani

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limetoa taarifa ya kulaani vikali shambulizi la Aprili 9 asubuhi, lililowaua walinda amani watano na wafanyakazi wengine wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS, na kutoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini kuchunguza haraka tukio hilo, na kuwawajibisha wahalifu kisheria. Wanachama wa Baraza hilo wametuma [...]

09/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM na Panasonic kuukabili ukatili wa kijinsia Somalia kwa taa za nishati ya jua

Kusikiliza / IOM na kampuni ya Panasonic kusaidia kukabili ukatili nyumbani

Je, ukatili wa nyumbani unaweza kukabiliwa kwa kutumia taa zinazotumia nishati ya miale ya jua? Hili ndilo linajaribiwa kutekelezwa sasa hivi nchini Somalia na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji likishirikiana na kampuni ya Kijapan ya Panasonic, kama anavyoarifu Joseph Msami (SAUTI MSAMI) Katika kupambana na ukatili wa kijinsia nchini Somalia, Shirika la kimataifa la masuala [...]

09/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani vikali mauaji ya walinda amani Sudan Kusini

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameelezea kushtushwa na shambulizi dhidi ya msafara wa walinda amani  wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini mapema Jumanne asubuhi. Bwana Ban amelaani vikali mauaji ya walinda amani 6 kutoka India na wafanyakazi wengine wawili wa UNMISS raia wa Sudan Kusini, na watano wa kikandarasi, katika eneo la [...]

09/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM yalaani vikali mauaji ya walinda amani na wafanyakazi wake Sudan Kusini

Kusikiliza / Majeruhi wa mashambulizi Sudan Kusini

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, amelaani vikali tukio la kuuwawa kwa askari watano waliokuwa kwenye kikosi cha ulinzi wa amani. Hilde Johnson amesema kuwa watumishi hao waliokuwa wakifanya kazi kwenye ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusin UNMISS walivamia na watu wasiojulikana wakati wakiwa karibu na makazi [...]

09/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uingereza kujitahidi kumaliza sintofahamu ya wasio na utaifa:UNHCR taa za miale ya jua

Kusikiliza / Nembo ya UNHCR

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limekaribisha hatua za kujidhatiti za Uingereza ambazo zimeanza kutekelezwa April 6 kukabiliana na tatizo la wasio na utaifa. Joshua Mmali na maelezo zaidi (SAUTI YA JOSHUA) Hatua hizo zinawaruhusu watu wasio na utaifa ambao kwa sasa wanaishi Uingereza kwa kujitenga na kukabiliwa na hatihati za kisheria [...]

09/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mwandishi wa UNMISS amuua mkewe na kujiua

Kusikiliza / UNMISS

Mwandishi wa habari aliyekuwa akifanya kazi katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa ajili yaSudanKusin UNMISS amejiua baada ya kutuhumiwa kuwa alimuua mkewe. Mke wa mwandishi huyo wa habari wa redio naye pia alikuwa ameajiriwa katika kituo alichokuwa akifanyia kazi mumewe. Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja chanzo cha matukio hayo na maafisa wa polisi [...]

09/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ITU  yazindua shindano kwa wabunifu vijana

Kusikiliza / ITU

Shirika la kimataifa la mawasilino ITU limezindua shindano lake ambalo hufanyika kila mwaka kwa shabaha ya kuchochea ubunifu kwenye sekta ya habari, mawasiliano na teknolojia. Washiriki wa shindano halo wanatakiwa kubuni miradi ya ujasilia malikupitia teknolojia ya mawasiliano na kisha kiwakilisha kwa jopo la wataalamu wa ITU wataokutana Novemba mwaka huu huko Bangkok. Shindano hilo [...]

09/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mjumbe maalumu wa UM ahitimisha ziara yake ya kwanza Somalia

Kusikiliza / Bi. Zainab Hawa Bangura

Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika unyanyasaji wa kingono kwenye maeneo yaliyokumbwa na machafuko Zainab Hawa Bangura  amekamilisha ziara yake ya kwanza nchini Somalia ambako amekutana na kufanya mazungumzo na makundi mbalimbali ya watu. Katika ziara yake hiyo Bi Bangura pia amekutana na mawaziri, Maafisa wa AMISOM, majaji na maafisa wa [...]

09/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Msaada wa madawa wawasili kwenye Jamhuri ya Afrika kati

Kusikiliza / Moja ya kambi za wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Ndege maalum ya shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF ikiwa imesheheni  tani 23 za madawa na matenki ya maji imewasili jana kwenye taifa linalokumbwa na mzozo la Jamhuri ya Afrika ya kati, majuma mawili baada ya waasi kuchukua uongozi wa taifahilo. Msaada huo unaojumuisha bidhaa muhimu  kwenda Jamhuri ya Afrika ya kati [...]

09/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watu 85 wameuawa huko Jongley, Sudan Kusini

Kusikiliza / Walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Jonglei

Ripoti ya Umoja wa Maataifa iliyochapishwa Ijumaa iliyopita inaonyesha kuwa karibu watu 85 waliuawa wakati wa uvamizi dhidi ya kundi moja la wafugaji karibu na eneo la Walgak kwenye jimbo la Jonglei tarehe 8 mwezi Februari mwaka huu wengi wakiwa ni wanawake na watoto. Assumpta Massoi anaripoti. (PKG YA ASSUMPTA) Kulingana na uchunguzi uliongoza na [...]

09/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hofu ya mafua ya H7N9 bado yaighubika China:WHO

Kusikiliza / Mtaalamu katika uchunguzi

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO  hadi sasa visa 24 vya mafua aina ya H7N9  vimebainika katika majimbo manne nchiniChinahuku watu 7 wakipoteza maisha kutokana na maradhi hayo. WHO inasema hakuna maambukizi baina ya binadamu kwenda kwa binadamu lakini mwenendo unafuatiliwa kwa karibu. Shirika la chakula na kilimo FAO na wizara ya kilimo [...]

09/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wakimbizi wa Syria kuzidi kuongezeka: UNHCR

Watoto wakimbizi kutoka Syria

Idadi ya raia wa Syria watakaotafuta hifadhi nchi jirani kwa mwaka huu wa 2013 inatarajiwa kuongezeka na kufikia Milioni Nne iwapo mzozo unaoendelea hivi sasa nchini mwao hautapatiwa suluhisho la kisiasa. Shirika la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR limesema kuwa hadi sasa Jordan, Uturuki, Lebanon na Iraq kwa jumla wanahifadhi wakimbizi zaidi ya Milioni Moja nukta [...]

09/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930