Nyumbani » 05/04/2013 Entries posted on “Aprili 5th, 2013”

Ban apokea tuzo kutoka Hispania, aiomba isaidie utatuzi wa mizozo

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepokea tuzo kuhusu masuala ya kiuchumi huko Hispania na kushukuru nchi hiyo kwa kutambua dhima ya Umoja wa Mataifa katika kujenga maendeleo, kulinda amani na utetezi wa haki za binadamu. Bwana Ban amesema Hispania imekuwa mshirika wa karibu wa Umoja wa Mataifa katika ajenda mbali mbali kuanzia maendeleo, [...]

05/04/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Msaada wa UNICEF kwa wakimbizi wa Syria Jordan uko njia panda:

Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema huenda likalazimika kusitisha ugawaji wa misaada ya kibinadamu kwa zaidi ya wakimbizi 100,000 wa Syria walioko Jordan kutokana na ukosefu wa fedha. UNICEF inasema ifikapo Juni mwaka huu halitokuwa na uwezo wa kutoa huduma za maji salama, usafi, chanjo, elilmu na ulinzi kwa wakimbizi wa [...]

05/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuelekea kikomo cha malengo ya milenia, Tanzania yapiga hatua dhidi ya Maleria.

Kusikiliza / Tanzania yapiga hatua dhidi ya ugonjwa, malaria

Zikiwa zimesalia takribani siku 1000 kabla ya kikomo cha malengo ya Milenia mwaka 2015, Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa mapambano dhidi ya magonjwa imepiga hatua katika kutokomeza ugonjwa wa Malaria unaotajwa kusababisha vifo kadhaa huku idadi kubwa ikiwa watoto walio chini ya umri wa miaka miatano. Ungana na George Njogopa katika makala inayoangazia juhudi [...]

05/04/2013 | Jamii: Mahojiano, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu Ban azungumza na Malala Yousufzai

Ban-Malala-300x214

05/04/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Siku ya afya duniani; Shinikizo la damu ni tatizo kubwa: WHO

Kusikiliza / Siku ya afya duniani 2013

Siku ya afya duniani, tarehe Saba mwezi Aprili mwaka huu wa 2013 imetajwa mahususi kumulika shinikizo la damu.  Shinikizo la damu limetajwa kuwa chanzo cha magonjwa mengi yanayohusiana na kushindwa moyo kufanya kazi yake. Shirika la afya duniani, WHO linaeleza kuwa mtu mmoja kati ya watu wazima watatu ana shinikizo la damu na wengi wao [...]

05/04/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UM waanza kuhesabu siku 1000 hadi kufikia malengo ya maendeleo ya milenia

Kusikiliza / Siku 1000 hadi kufikia MDGs

Umoja wa Mataifa umeanza leo kuhesabu siku elfu moja hadi kufikia tarehe ya mwisho ya kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia. Katika ujumbe wake wa awali, Katibu Mkuu Ban Ki-moon, amesema juhudi zaidi zinatakiwa ili kutimiza malengo yalosalia, akisisitiza kuwa njaa na utapiamlo vinaweza kutokomezwa. Naye, Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa idadi ya watu, UNFPA [...]

05/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Malala Yousfzai azungumza na Ban, amwelezea afya yake

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon katika mazungumzo na Malala Yousfzai kwa njia ya mtandao

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo kwa njia ya mtandao na mtoto Malala Yousfzai ambaye alijeruhiwa kwa risasi na watalibani huko Pakistani mwezi Oktoba mwaka jana kutokana na msimamo wake wa kutetea bayana elimu kwa mtoto wa kike. Katika mazungumzo hayo Bwana Ban ameelezea kufurahishwa kwake kwa kumuona Malala akiwa mwenye [...]

05/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahabusu ya Guantanamo ifungwe:Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Navi Pillay Ijumaa amevitaka vitengo vyote vya serikali ya Marekani kufanyakazi pamoja ili kufunga kituo cha mahabusu cha Guantanamo akisema kuendelea kuwashililia mahabusu bila hukumu ni ukiukaji wa sheria za kimataifa. Amesema amesikitishwa na kitendo cha serikali ya Marekani kutoweza kufunga kituo cha Guantanamo Bay [...]

05/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Sera za uchimbaji madini zimeengua wanawake: Waziri Simba

Kusikiliza / UN-Women

Mkutano wa siku mbili wa ngazi ya mawaziri ulioangalia suala la jinsia kwenye sekta ya madini umemalizikaTanzania. Shirika la Umoja wa Mataifa la wanawake, UN-Women liliandaa mkutano huo kwa ushirika na Publish What You Pay. Washiriki walikubaliana kuwa wakati umefika wanawake washiriki kwa kina kwenye sekta hiyo. Miongoni mwao ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, [...]

05/04/2013 | Jamii: Mahojiano, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wakimbizi wa Mali nchini Niger yaongezeka upya

Kusikiliza / malirefugees

Takriban wakimbizi 5,600 kutoka Mali wamevuka mpaka na kuingia Niger wiki ilopita. Wakmibizi hao ambao walisafiri kwa miguu na kwa kupanda punda, wanatoka maeneo ya Kidal na Menala, na wengi wao ni wanawake na watoto. Wanasema walikimbia hasa kwa sababu ya mapigano yanayoendelea kaskazini mwa Mali na kwa sababu wanaogopa uwezekano wa ulipizaji kisasi wa [...]

05/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yasikitishwa na vurugu zilizotokea kwenye kituo kimoja Indonesia

Kusikiliza / UNHCR logo

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa limevunjwa moyo na kusikitishwa kufuatia taarifa za kuzuka kwa hali ya sintofahamu kwenye kituo cha Medan kilichoko Kaskazini mwa jimbo la Sumatra nchini Indonesia. Duru za habari zinasema kuwa, kituo hicho kilikumbwa na machafuko yaliyohusisha waomba hifadhi na jamii ya watu wa Myanmar. Watu [...]

05/04/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Shughuli maalumu za kuchagiza amani zazileta pamoja jamii za Sudan Kusini:IOM

Kusikiliza / south sudan

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM linaendesha shughuli maalumu za kuchagiza amani Sudan Kusini. Lengo ni kuzileta pamoja jamii za taifa hilo ili kushirikiana na kutumia pamoja rasilimali zilizopo wakati huu ambapo machafuko ya kijamii yanaendelea. Jumbe Omari Jumbe msemaji wa IOM anafafanua zaidi: (SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)  

05/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wasikitishwa na ongezeko la adhabu ya kifo

Kusikiliza / Rupert Colville

  Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu imesema nchi nyingi za Mashariki ya Kati na bara la Asia zimepuuza wito wa kusitishwa kwa adhabu ya kifo na kunyonga wahalifu, na zinaendelea kutekeleza adhabu hiyo inayokiuka misingi ya haki za binadamuTaarifa zaidi na Joseph Msami: TAARIFA YA MSAMI Kwa mujibu wa Ofisi ya [...]

05/04/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wasitisha ugawaji wa chakula Gaza:

Kusikiliza / unrwafood

Umoja wa Mataifa umesitisha kwa muda mipango yote ya ugawaji wa chakula Gaza baada ya waandamanaji kuvamia moja ya vituo vya kama inavyoarifu taarifa iliyoandaliwa na Flora Nducha. (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Shirika la Umoja wa mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema uvamizi uliofanyika kwenye moja ya vituo vya Gaza ambao unaonekana [...]

05/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mzozo Jamhuri ya Afrika ya Kati wasababisha maelfu ya wakimbizi

Kusikiliza / CAR

Mashirika ya kutoa misaada yanaripoti kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wanaokimbilia nchi jirani. Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema idadi ya wakimbizi hao imepanda na kuzidi 37, 000 katika wiki chache zilizopita, wengi wao wakikimbilia Chad, Cameroon, na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC). UNHCR [...]

05/04/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031