WFP na UNHCR yapokea msaada kwa ajili ya kambi ya Nyarugusu

Kusikiliza /

Nyarugusu, Kasulu, Kigoma

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la wakimbizi UNHCR na lile la Mpango wa Chakula duniani WFP yamepokea msaada wa Dola Milioni Saba kutoka serikali ya Japan  kwa ajili ya kambi ya Nyarugusu iliyoko wilaya ya Kasulu, Kigoma, magharibi mwa Tanzania.

Kambi hiyo ni ya mwisho miongoni mwa kambi zinazohifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

Mellanie Senelle ni msemaji wa UNHCR na amefafanua matumizi ya msaada huo ikiwemo kuimarisha lishe bora.

SAUTI (MELLANIE)

''Msaada huu toka Japan utasaidia wakimbizi katika maeneo muhimu ya afya ya msingi kama vile maji,malazi,lakini pia kuna malengo muhimu ya kielimu kuwasaidia watoto kujiunga elimu ya msing, .Pia tutasaidia wakimbizi wenye mahitaji maalum kama wazee,walemavu,wenye magonjwa sugu na wajawazito.''

Halikadhalika msemaji huyo wa UNHCR amezungumzia namna UNHCR itakavyosaidia waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi katika kambi ya Nyarugusu

(SAUTI YA MELLANIE)

''UNHCR inafanya kazi na washirika wengine ambao wamejikita katika masuala ya   afya kama HIV, masuala ya elimu ya kinga,na kubadili tabia. Kwa hiyo msaada huu tutautumia kuboresha maisha ya waathirika wa ugonjwa hu''.  

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031