Wataka kupitishwa mkataba wa udhibiti wa silaha

Kusikiliza /

Irene Ado Torshie

Makundi ya wabunge duniani kote wametoa mwito kufikiwa makubaliano juu ya mkataba wa udhibiti wa biashara ya silaha, katika wakati ambapo viongozi kutoka pande mbalimbali wakitarajia kuanza kukutana hapo alhamisi kwa ajili ya kujadilia kama kuwepo makubaliano ya pamoja juu ya kufikiwa kwa mkataba huo au la.

Mmoja wa wabunge hao Irene Torshie kutoka nchini Ghana amepigia upata kuhusu kuwepo kwa mkataba huo akisema kuwa utasaidia kusimamia mwenendo wa uuzaji wa silaha duniani.

Amesema dunia inapaswa kuwa na utashi wa pamoja ili kuhakikisha kwamba mwenendo wa silaha hautumbukia mikononi mwa watu wasiitakia mema dunia na hivyo amewahimiza wajumbe wanaokutana kwa ajili ya kujadilia mkataba huo kutambua wajibu waliopewa na jamii.

Maelfu ya wajumbe wanaowakilisha serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya kimataifa wamekutana juma hili kwa ajili ya kutayarisha mkataba huo ambao unatazamiwa kuanza kujadiliwa siku ya alhamisi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2014
T N T K J M P
« ago    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930