Wataalam wa UM wakerwa na mauaji ya watu 7 Saudi Arabia

Kusikiliza /

Wataalam wawili huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji yasiyo halali, utesaji na vifungo vya ovyo, leo wameeleza kukerwa na mauaji ya wanaume saba nchini Saudi Arabia, licha ya wito wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya umma wa kuitaka mamlaka ya Saudia  isitekeleze mauaji hayo.

Mauaji hayo ambayo yametekelezwa Jumatano asubuhi, yamefanywa kwa kuwapiga risasi wanaume hao, badala ya kuwachinja kama ilivyo kawaida nchini humo.

Christof Heyns, ambaye ndiye mtaalam maalum kuhusu mauaji yasiyo halali, amesema amesikitishwa sana na mauaji hayo, na kusisitiza kuwa, mauaji yoyote yanayotekelezwa kinyume na wajibu wa kila taifa chini ya sheria za kimataifa, yanachukuliwa kuwa mauaji ovyo na kinyume na sheria.

Mtaalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu utesaji wa watu, Juan E. Méndez, ameelezea kusikitishwa na madai kuwa watu hao saba waliteswa wakiwa kizuizini na kulazimishwa kutia saini maandishi ya kukiri kabla ya kuuawa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031