Wakazi wa Jonglei wakimbilia mtoni kuokoa maisha yao: OCHA

Kusikiliza /

Wakazi wa Jonglei waliokimbia makazi yao

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA ,  nchini Sudan Kusini ,  imetoa taarifa kuhusu usalama wa wakazi wa jimbo la Jonglei kufuatia  mapigano kati ya majeshi ya serikali na vikundi vyenye  silaha ambapo baadhi ya watu wamejeruhiwa huku wengine wakikimbilia misituni. Katika taarifa yake OCHA imesema watu kadhaa wamekimbia na kujificha kweney mito ikiwemo mto Keng Keng huku wengine wakitafuta hifadhi kwenye ofisi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo hilo.   OCHA inasema uwepo wa vikundi kadhaa vyenye silaha kwenye eneo hilo unaibua wasiwasi wa uwezekano wa mashambulizi ya kijeshi ya kulipiza kisasi na mashirika ya misaada yameandaa mipango ya kutoa misaada kwa kuweka vifaa vyao huko Boma na Pibor. OCHA imetaka pande zote kuheshimu sheria za kimataifa za usaidizi wa binadamu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031