Vitendo sasa vyahitajika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake: Ban

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM, Ban Ki-Moon katika shughuli maalum ya siku ya wanawake duniani, “Ahadi ni Ahadi”.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe wa siku ya wanawake duniani hii leo na kutaka kila mtu kwa nafasi yake kusongesha mbele jitihada za kimataifa za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike ili kundi hili liweze kuishi huru na katika mazingira salama na yenye ulinzi.

Bwana Ban amesema katika siku hii kila mtu anapaswa kuangalia mwaka uliopita uliogubikwa na uhalifu wa kutisha wa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake kuanzia msichana kubakwa na kundi la watu hadi kufa na watoto wa kike kupigwa risasi kwa sababu ya kutafuta elimu.

Katibu Mkuu huyo pamoja na kuunga mkono hatua zinazochukuliwa na serikali na taasisi za kiraia katika kupambana na vitendo hivyo amesema wakati umefika wa kuchukua hatua kali dhidi ya wale wanaofanya vitendo hivyo dhalili dhidi ya wanawake.

Na katika shughuli maalum iliyofanyika leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani na kushuhudiwa uzinduzi wa wimbo maalum wa mwanamke, Bwana Ban amesema ahadi ya kulinda wanawake dhidi ya ukatili ni lazima itekelezwe.

(SAUTI YA BAN)

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031