Vijana wanaweza kusaidia kukabiliana na changamoto za sasa duniani,Ban

Kusikiliza /

Katibu Mkuu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki- moon amezungumza katika kongamano la vijana kuhusu ushauri wa kiuchumi na kijamii na kusema licha ya changamoto wanazokabiliana nazo vijana wana fursa ya kuleta mabadiliko duniani.

Ban amesema vijana wana mawazo na nguvu za kukabiliana na changamoto ikiwamo ukosefu wa ajira tatizo alilosema linawakabili karibu watu milioni 74 kote duniani, waathirika wakubwa wakiwa ni vijana na kuongeza kuwa migogoro huliathiri kundi hilo na kusababisha kupoteza nyumba, familia zao kuharibu maisha ya badaye.

Hata hivyo Bwana Ban amesema ni jukumu la Umoja wa Mataifa kunoa utaalamu walionao vijana ili watimize malengo ya ya kutatua matatizo sugu katika dunia.

(SAUTI YA BAN)

'' Munaweza kutusaida kukabili changamoto kwa kuwa raia wa ulimwengu. Lazima tufanye kazi dhidi ya mgawanyiko wa kidijitali. Ni lazima tutoe fursa kwa wanawake na wasichana. Wana uwezo sawa na wanaume na wavulana katika swala la sayansi na teknolojia. Umoja wa Mataifa uko tayari kushirikiana nanyi. Ndiyo maana nimeteua ujumbe wa kwanza na kipekee wa vijana. Munapofanya kazi kwa ajili ya dunia njema kwa wote munajenga maisha mema badaye kwa ajili yenu pia ''

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031