Ushirikiano zaidi wahitajika kudhibiti matumizi ya maji: Jeremic

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Rais wa Baraza Kuu la UM Vuk Jeremic

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Vuk Jeremic, amesema ni vigumu kutokomeza umaskini na kuhakikisha afya nzuri bila maji safi na salama.  Akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza Kuu kuhusu ushirikiano kuhsu maji, Bwana Jeremic amesema maji ndicho chanzo cha uhai, na wakati huu wa kuadhimisha mwaka wa kimataifa wa ushirikiano kuhusu maji, ulimwengu unatakiwa kuungana ili kukubaliana kuhusu jinsi ya kushirikiana kwa matumizi ya maji.

(SAUTI YA JEREMIC)

 "Maji ni nguzo ya maendeleo endelevu, kwani yanahusiana kwa karibu sana na changamoto muhimu za kimataifa. Idadi ya watu inapoongezeka na kuongezeka kwa mahitaji ya matumizi vinaongeza shinikizo katika uzalishaji wa maji na nishati. Katika siku zijazo, maji yatahitaji kudhibitiwa kwa njia endelevu zaidi" 

 Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema maji ndiyo yanayoshikilia ufunguo wa maendeleo endelevu, katika ujumbe wake wa kuadhimisha Siku ya Maji Duniani. Amesema tunahitaji maji kwa afya, usalama wa chakula na maendeleo ya kiuchumi.  Licha ya umuhimu huu, Bwana Ban amesema kila mwaka, mashinikizo mapya ya matumizi ya maji yanaingia.

Amesema, kila mmoja kati ya watu watatu, anaishi katika nchi isiyo na maji ya kutosha, na ifikapo mwaka 2030, huenda nusu ya idadi ya watu kote duniani ikakumbwa na uhaba wa maji, huku mahitaji yakizidi uzalishaji kwa asilimia 40.

(SAUTI YA BAN)

Maji yanashikilia ufunguo wa maendeleo endelevu: Ban

 

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema maji ndiyo yanayoshikilia ufunguo wa maendeleo endelevu, katika ujumbe wake wa kuadhimisha Siku ya Maji Duniani. Amesema tunahitaji maji kwa afya, usalama wa chakula na maendeleo ya kiuchumi.

Licha ya umuhimu huu, Bwana Ban amesema kila mwaka, mashinikizo mapya ya matumizi ya maji yanaingia.

 

Amesema, kila mmoja kati ya watu watatu, anaishi katika nchi isiyo na maji ya kutosha, na ifikapo mwaka 2030, huenda nusu ya idadi ya watu kote duniani ikakumbwa na uhaba wa maji, huku mahitaji yakizidi uzalishaji kwa asilimia 40.

 

(SAUTI YA BAN)

 "Wakati tunapobuni ajenda ya maendeleo baada ya 2015, lengo letu ni kutokomeza umaskini ulokithiri na njaa, na kujenga ulimwengu wenye nafasi sawa kwa wote. Ili kutimiza hayo, ni lazima tuzingatie kwa njia ya usawa suala la mazingira katika maendeleo endelevu. Hatuwezi kuendelea bila maji safi nay a kutosha. Kwenye Siku hii ya Maji Duniani, natoa mwito wa ushirikiano zaidi. Tutumie maji kwa busara, bila kuyaharibu, ili kila mtu ayapate."

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031