UNWRA yalaani mauaji ya watoto wa Kipalestina nchini Syria

Kusikiliza /

Mtoto wa kipalestina

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uratibu wa misaada ya usamaria mwema kwa wakimbizi wa Kipalestina UNWRA, limelaani vikali tukio la mauaji ya wakimbizi watoto watano wa kipalestina nchini Syria na kuonya uwezekano wa mzozo huo kuvuruga ustawi wa vijana.  Kulingana na taarifa za UNWRA,kuuawa kwa watoto hao kunazidisha hali ya wasiwasi juu ya kupanuka zaidi kwa mapigano hayo ambayo sasa yameingia hata kwenye kambi za wakimbizi wa Kipalestina nchini Syria.  Shirika hilo limesema kuwa mauaji hayo yanashukiza na kuzusha hali ya wasiwasi zaidi juu ya ustawi wa watoto na raia wa kawaida. Limetoa mwito kwa pande zote zinazozozana kuheshimu sheria za kimataifa ambazo zinataka kulindwa kwa makundi ya watu yasiyofungamana na upande wowote kwenye mzozo huo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031