UNAIDS yakaribisha habari za mtoto "kupona" baada ya matibabu dhidi ya HIV

Kusikiliza /

 

Ukimwi barani Afrika

Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa juu ya ugonjwa wa Ukimwi (UNAIDS) leo umekaribisha ripoti ya utafiti kuhusu mtoto aliyetibiwa kwa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa Ukimwi saa thelathini baada ya kuzaliwa na kisha kuacha matibabu hayo lakini akapatikana hana tena maambukizi.

Kwa mujibu wa utafiti huo mama mzazi wa mtoto huyo hajawahi kupata tiba ya kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi. Ripoti ya utafiti huo itawasilishwa leo katika kongamano juu ya Maambukizi na Kinga mjini Atlanta, Georgia nchini Marekani. Taarifa zaidi na Joseph Msami

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2013
T N T K J M P
« apr    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031