Ukata watia hatarini harakati za kudhibiti Kifua Kikuu

Kusikiliza /

Mtoto akiwa katika moja ya wodi za tiba dhidi ya Kifua Kikuu huko Phillipines

Shirika la afya duniani WHO na mfuko wa kimataifa wa kupambana na ugonjwa wa ukimwi, kifua kikuu na Malaria yanasema ugonjwa wa kifua kikuu ulio sugu kwa dawa,  unazidi kuenea na kwamba karibu dola bilioni Moja nukta Sita zahitajika kial mwaka kwa tiba dhidi ya ugonjwa huo.  Wakizungumza mjini Geneva kabla ya maadhimisho ya siku ya kifua kikuu dunaini tarehe 24 mwezi huu, wakuu wa mashirika hayo mawili wanasema njia pekee ya kutekeleza kinachohitajika ni kubaini visa vyovyote vya ugonjwa wa kifua kikuu na kukabiliana vilivyo huku wakisema vyanzo vya ndani vya fedha pia ni muhimu kwa tiba endelevu.  Wanasema kuwa kuwepo kwa kifua kikuu sugu kijulikanacho kama MDR-TB ni jambo linaloleta changamoto zaidi wakati huu ambapo . Dr Margaret Chan ni mkuu wa WHO.

(SAUTI Dkt. Chan)

"Tunatwanga maji kwenye kinu, wakati ambapo tunahitajika kuchukua hatua kukabiliana na ugonjwa sugu wa MDR-TB. Tumechukua hatua zinazohitajika katika kuzuia ugonjwa wa kifua kikuu kutokana na ushirikiano wa kimataifa, lakini  tunaweza kupoteza mafanikio yote kama hatutachukua hatua sasa. "

Kwa upande wake Dkt. Mark Dybul, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Fund amesema changamoto ni kufikia wananchi wa pembezo kama vile wafungwa, watumiaji wa madawa ya kulevya ambao mara nyingi huenguliwa katika mfumo halisi wa tiba.

 (SAUTI Dkt. Mark)

"Utashi wa kisiasa unahitajika ili kuwapatia tiba  watu wasio na uwezo na wale wa pembezoni. Lakini pia utashi wa kisiasa ni muhimu ili kutenga bajeti kutoka vyanzo vya ndani vya fedha."

 

Huku malengo ya milenia ya kumaliza ugonjwa wa kifua kikuu yakiwa yametimizwa baadhi ya maeneo, bara la Afrika na Ulaya yameelezwa kutokuwepo kwenye mkondo wa kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo kwa asilimia hamsini ifikapo mwaka  2015.

 

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031