Ubaguzi hauna nafasi dunia ya leo amesema Dkt. Bana

Kusikiliza /

Baraza Kuu

Mapema wiki hii Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilifanya hafla maalum ya kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya waathirika wa utumwa na biashara ya utumwa ya bahari ya Atlantiki, ambapo akizungumzia minajili ya biashara hiyo, mchambuzi wa siasa za kimataifa, mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Dar es salaam idara ya Sayansi ya siasa na utawala Dk Benson Bana amesema ubaguzi wa aina yoyote hauna nafasi katika dunia ya leo.

Katika mahojiano maalum na radio ya Umoja wa Mataifa Dkt. Bana amesema sehemu kubwa ya jamii sasa inafahamu maana ya usawa miongoni mwa binadamu wote.

(SAUTI YA DK BANA)

Siku ya kimataifa ya kumbukumbu ya biashara ya utumwa hufanyika kuchagiza ufahamu juu ya athari za ubaguzi wa rangi na aina nyingine za ubaguzi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031