Tuko tayari kusaidia uchunguzi wa ripoti za matumizi ya silaha za kemikali Syria: Pillay

Kusikiliza /

Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amekaribisha uamuzi wa Katibu Mkuu Ban Ki-moon kufanya uchunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu madai kwamba huenda silaha za kemikali zimetumiwa nchini Syria.  Bi Pillay amesema ofisi ya haki za binadamu i tayari kusaidia katika uchunguzi huo.Hadi sasa hakuna ushahidi mkubwa unaoonyesha kwamba silaha za kemikali zimetumiwa. Hata hivyo, msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu, Rupert Colville, amesema ikigunduliwa kuwa kweli silaha za kemikali zimetumiwa, hicho kitakuwa kitendo kiovu mno na kosa la lisilokubaliwa kabisa.

(RUPERT COLVILLE 32")

"Tunatumai ripoti hizi si sahihi, kwani ikiwa ni za kweli, basi mzozo huu utakuwa umezama na kufikia viwango vipya. Matumizi ya silaha za kemikali bila shaka utakuwa uhalifu wa dhidi ya ubinadamu au uhalifu wa kivita. Kamishna Mkuu anaunga mkono ujumbe wa Katibu Mkuu kwamba kwamba ikiwa uhalifu kama huo umetendeka, wahusika ni lazima wawajibike kisheria. Wakati matokeo ya uchunguzi yakisubiriwa, Kamishna Mkuu anarudia mwito wake kwa pande zote katika mzozo kukomesha mara moja mashambulizi dhidi ya raia, na kuhakikisha usalama wao."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29