Theluthi mbili ya wanaokabiliwa na hatari ya mabomu ya ardhini nchini Mali ni watoto.: UNICEF

Kusikiliza /

Wanawake nchini Mali wakiwa kwenye foleni wakisubiri watoto wao wapimwe afya

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limetahadharisha kuhusu hatari inayozikumba jamii kati na kaskazini mwa Mali,  hatari inayotokana na risasi na mabomu ya ardhini.

Tangu mwezi Aprili mwaka uliopita visa 60 vinavyohusiana na mabomu ya ardhini vimeripotiwa huku visa  miongoni mwa watoto vikichukua theluthi mbili ya visa vyote. Kati ya visa hivyo watu 53 walijeruhiwa , wakiwemo watoto 38 na watu wazima 15 huku saba wakiuawa wakiwemo watoto watano na watu wazima wawili.

UNICEF inasema kuwa hatari iliyopo inatarajiwa kuongezeka zaidi wakati familia zilizohama makwaa zitakapoanza kurudi nyumani kwenye maeneo ambayo awali yamekumbwa na mapigano. Msemaji wa UNICEF, Marixie Mercado, amesema kuwa mnamo mwezi Disemba UNICEF ilikadiria kuwa karibu watoto 100,000 na wazazi walikabiliwa na hatari ya mabomu hayo kaskazini na Mali.

 

(SAUTIO YA MARIXIE MERCADO)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031