Sierra Leone yaishukuru UM kwa kuunga mkono juhudi za amani

Kusikiliza /

Bendera ya Sierra Leone

Serikali ya Sierra Leon imetoa taarifa ikizishukuru taasisi za kimataifa ikiwemo utendaji kazi wa Umoja wa Mataifa ambao umesaidia pakubwa ustawi wa taifa hilo

Balozi wa Sierra Leone kwenye Umoja wa Mataifa  Shekou Touray, amesema kikosi maalumu  cha kimataifa kilichopo nchini humo kwa ajili ya ulinzi wa amani, kimesaidia pakubwa ujenzi wa maridhiano.Mapema siku ya jumanne, Baraza la Usalama lilipitisha azimio linalotaka kurefushwa muda wa kuwepo kwa vikosi hivyo nchini Siera Leona ili kutekeleza baadhi ya majukumu.

Miongoni mwa majukumu hayo ni pamoja na kuendelea kuipiga jeki serikali inayoendesha mchakato wa mapitio ya katiba na kuunga mkono harakati zinazokaribisha majadiliano ya kisiasa kwa shabaha ya kumaliza kabisa mikwamo ya kisiasa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031