Mzozo wa Syria unakiweka kizazi kizima cha watoto mashakani: UNICEF

Kusikiliza /

watoto, Syria

Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limeonya kuwa kizazi kizima cha watoto wa Syria kipo mashakani, wakati mzozo wa Syria ukiingia mwaka wa tatu.

Katika ripoti yake ilotolewa leo ambayo ni tarehe ya kutimu miaka miwili tangu mzozo wa Syria kuanza, UNICEF imesema kuwa kukithiri kwa machafuko, uharibifu mkubwa wa miundo mbinu pamoja na halaiki ya watu kuachwa bila makazi, vinakiacha kizazi kizima cha watoto na kovu la maisha.

Zaidi ya watoto milioni mbili wameathiriwa na mzozo wa Syria katika eneo zima la Mashariki ya Kati. Ripoti ya UNICEF pia inasema katika maeneo yaloathiriwa zaidi na mapigano, huduma za maji zimeathirika kwa thuluthi mbili na kuongeza magonjwa ya ngozi na mapafu, huku moja kati ya kila shule tano zikiaribiwa au kutumiwa kama makazi ya wakimbizi wa ndani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031